Kampuni ya Sony Pictures imesema kuwa sinema yenye utata ya ucheshi kuhusu namna ya kumuuwa kiongozi wa Korea Kaskazini, imewekwa katika mitandao Nchini Marekani.
Kampuni hiyo inasema kuwa imechagua njia ya kusambaza sinema hiyo kupitia mitandao ya digitali, ili kuruhusu watu wengi zaidi kutizama sinema hiyo iitwayo, 'The Interview'.
Uzinduzi wa awali wa filamu hiyo ulizingirwa na utata wa mashambulizi ya kimitandao ambapo Marekani ililaumu Korea Kaskazini kwa hitilafu hiyo. BBC
Post a Comment