Rais Robert Mugabe ameteuliwa tena kuongoza chama tawala nchini Zimbabwe na mke wake Grace akapewa wadhifa wa juu katika chama.
Kupandishwa cheo kwa Grace Mugabe kuongoza tawi la wanawake la Zanu-PF kunamuweka katika nafasi nzuri ya kumrithi mumewe katika siku zijazo,wanasema wachambuzi.
Mke huyo wa Rais amewashtumu wakinzani wake wa kisiasa akiwemo Makamo Rais Joyce Mujuru, katika miezi ya hivi karibuni.
Bwana Mugabe mwenye umri wa miaka 90,anatazamiwa kugombea tena urais mnamo mwaka 2018.
Akizungumza katika mkutano mkuu wa Zanu-PF,Bwana Mugabe aliwashukuru maelfu ya wafuasi wake kwa kumchagua kuongoza chama . "Najua nilikotoka.. mimi si bora kushinda watu walonizaa ," alisema Mugabe, ambaye ameiongoza Zimbabwe tangu mwaka 1980.
Madai ya mauaji
Kuteuliwa kwa mke wa Mugabe kuongoza tawi la wanawake kunaonekana kama ni ishara nyigine zaidi kwa Joyce Mujuru ambae wakati mmoja alionekana kama angeweza kumrithi Mugabe sasa amepigwa pande.
Bi Mujuru alipigania pamoja na Bw.Mugabe uhuru wa Zimbabwe kutoka utawala wa wazungu wachache.
Lakini alijikuta matatani wakati Bi Mugabe mwenye umri wa miaka 49, kujitumbukiza katika siasa mnamo mwaka huu na kumshutumu makamo wa rais wa kula njama dhidi ya mumewe.
Post a Comment