Mwaandishi
habari Mmarekani Luke Somers na mwalimu raia wa Afrika Kusini Pierre
Korkie wameuwawa na wapiaganaji wa al-Qaeda nchini Yemen katika juhudi
za kuwaokoa.
Peresheni ya kuwaokoa iliongozwa na vikosi maaulum vya Marekani na Yemen katika jimbo la kusini la Shabwa.
Rais wa Marekani Barack Obama alilaani kile alichokieleza "mauaji ya kinyama" ya mateka hao wawili.
Walikua
wanazuiliwa na wapiganaji wa kundi la al-Qaeda katika Bara arabu ambalo
Marekani inalichukulia kuwa mojawapo wa matawi hatari duniani ya kundi
kuu la al-Qaeda.
Kundi hilo lina makao yake Mashariki ya Yemen na
limeweza kupata wafuasi wengi katika nchi masikini iliokumbwa na
machafuko tangu kupinduliwa kwa Rais Ali Abdullah Saleh in 2011.
Maofisa wa ngazi za juu nchini
marekani wameiambia BBC kua vikosi maalum vilivyoshiriki katika jitihada
za kumuokoa Luke Somera nchini hawakuwa wanafahamu kuhusu mateka
mwingine aliyekuwa akishikilwa na wanamgambo hao.
Shirika ambalo
mwalimu huyo raia wa Afrika Kusini Pierre Korkie alikuwa akilifanyia
kazi lilisema kuwa mateka huyo angeachiliwa leo jumapili kufuatia
maafikiano ya kulipa fidia.
Marekani iliamrisha kuchukuliwa jitihada hizo kwa kuwa iliamini kwamba maisha ya bwana Somers yalikuwa hatarinibbc
Post a Comment