skendo inayovuma katika msimu huu wa Krismasi, umeipata hiyoo ni shidaaaa

 Ni Escrow kila kona



Dar/mikoani. Kashfa ya uchotaji wa fedha katika Akaunti ya Tegeta Escrow inayoendelea kulitingisha Taifa, jana ilitawala mahubiri ya Sikukuu ya Krismasi katika makanisa mbalimbali nchini, viongozi wa dini wakionyesha kutoridhishwa na maelezo na hatua zinazochukuliwa.


Wakihutubia waumini wao, viongozi hao walitumia siku hiyo kukemea vitendo vya ufisadi, wizi na uzembe.


Hofu ya Escrow


Ujumbe wa Askofu wa Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT) wa Kanisa la Anglikana, Dk Dickson Chilongani ulilenga kueleza hofu ya wananchi kutokana na sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow, ugumu wa maisha, ukosefu wa ajira, kukosa uhakika wa huduma bora za matibabu na elimu pamoja na wimbi la viongozi waandamizi wasiokuwa waaminifu na waadilifu.


Akihubiri katika Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu mjini Dodoma, Askofu Chilongani alisema mbali na maisha ya ufukara na ukosefu wa huduma, sakata la Escrow na hotuba ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa Jumatatu vimezidi kuzidisha hofu kwa Watanzania na kuwafanya waonekane kama hawana tumaini.


Akitumia mtindo wa kuhoji, Askofu Chilongani alianza kwa kuhoji, “Kitu gani kinakutia hofu unaposherekea sikukuu hii, watu wengi tunaishi katika ulimwengu wa hofu kutokana na ufukara, ukosefu wa huduma, tunajiuliza tutawasomeshaje watoto wetu, tutapataje huduma bora za matibabu, yaani kila mmoja wetu ana hofu,” alisema.


Askofu Dk Chilongani alisema ingawa kila mtu ana hofu yake lakini sakata la akaunti ya Escrow limejenga hofu kwa mwananchi, kila mmoja akihoji na kutengeneza majibu yake jambo linalotoa picha kuwa jibu sahihi halijatolewa au kupatikana.


“Mimi siyo mwanasiasa wala mtaalamu wa masuala ya siasa lakini kuna hili sakata la Escrow ambalo juzijuzi Rais amelitolea ufafanuzi, hili nalo linazidi kuwajengea wananchi hofu, wengine wanakosoa maazimio ya Bunge, wengine wanataka Serikali itoe maamuzi yenye tija kwa umma, yaani ni hofu tu,” alisema.


Escrow ni fedha za umma


Mchungaji wa Kanisa la Maombezi, Anthony Lusekelo alisisitizia kuwa fedha zilizochotwa katika Akaunti ya Tegeta Escrow ni mali ya umma kutokana na taarifa iliyowasilishwa na PAC bungeni.


Kauli hiyo inakuja baada ya Rais Kikwete kusema fedha hizo ni mali Kampuni ya IPTL na zilikuwa Sh202 bilioni na si Sh306 bilioni kama inavyodaiwa. Akihubiri katika kanisa hilo jana, Lusekelo maarufu kama ‘Mzee wa Upako’ alisema: “Niliisikiliza kwa makini mwanzo hadi mwisho (hotuba ya Rais) leo nimeona niseme machache kwamba fedha hizo ni mali ya umma. Mimi siungani na hao wanaodai fedha hizi siyo za umma lakini kwa hali hii hakuna jinsi inabidi tumwachie Mungu maana yeye ndiye atakayeweza kutuvusha kutoka hapa tulipo,” alisema mwananchi

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top