Steven Gerrard aibeba Liverpool FA, check hapa magoli yake

  

 
  bofya hapa chini kucheki video


 
Steven Gerrard ameonyesha ubora na uongozi na Liverpool itamkosa mchezaji wa aina hii wakati atakapohama Anfield.
Ni Gerrard aliyewainua mara mbili vitini mashabiki wa Liverpool ilipoizamisha AFC Wimbledon mabao 2-1 katika michezo inayoendelea ya Kombe la FA.
Gerrard, akicheza mchezo wake wa kwanza tangu atangaze kuihama Liverpool katika msimu ujao na kwenda kukipiga Marekani, alionyesha pengo atakaloliacha atakapoihama timu yake aliyokulia na kupata mafanikio makubwa.
Nahodha huyo wa Liverpool ambaye atasherehekea miaka 35 katika siku ya mwisho ya Kombe la FA, tarehe 30 mwezi Mei aliiongoza timu 30Liverpool's captain, who will celebrate his 35th birthday on FA Cup hiyo kupata mafanikio na amefanya hivyo mara nyingi wakati timu ilipojikuta katika matatizo.
Gerrard alianza kuichezea Liverpool mwaka 1998. Gerrard amefunga magoli 182 katika michezo 696 aliyoichezea timu ya Liverpool.
Na katika mchezo mwingine Tottenham walitoka sare na Burnley kwa kufungana goli 1-1. Burnley ndio waliokuwa wenyeji wa mchezo huo. bbc

JB AAMUA KUJIMALIZA

Muigizaji mkongwe kwenye filamu nchini, Jacob Steven ‘JB’.

Stori: Shani Ramadhani
MUIGIZAJI mkongwe kwenye filamu nchini, Jacob Steven ‘JB’ ameamua kujipoteza kwa makusudi katika uigizaji akiwa na lengo la kuweka mbele kazi zinazofanywa na kampuni yake ya uzalishaji sinema ya Jerusalemu.

Akipiga stori na gazeti hili, JB alisema mwaka 2014 filamu zake tatu za Bado Natafuta, Wageni Wangu na Chausiku zilifanya vizuri sokoni.

“Kwa asilimia 80 mwaka huu kwangu umekuwa mzuri kikazi, nimefanya kazi nzuri bila mimi kuonekana kwa sababu nataka Jerusalemu ianze halafu mimi baadaye ndiyo sababu kubwa iliyofanikisha muvi zangu zote kufanya vizuri, sitaki kuwa naonekana mara kwa mara kwenye filamu,” alisema. BY GP

R.I.P WASANII WETU! KINACHOWAUA KWA KASI CHAJULIKANA



MWAKA 2014 unakatika, matukio ya kukumbukwa ni pamoja na wasanii Bongo kupoteza maisha katika mazingira yasiyotarajiwa, Ijumaa linakupa hatua kwa hatua.Kumbukumbu za haraka zinabainisha kuwa, tangu mwaka 2011 mpaka 2014, wasanii wenye majina makubwa na madogo wasiopungua 32 wamefariki dunia kwa sababu mbalimbali.

Recho Haule enzi za uhai wake.

Inauma sana! Katika kipindi cha miaka mitatu kuwapoteza wasanii kwa kiasi hicho ni pigo kubwa kwa tasnia, hasa filamu na muziki, ukiwemo wa muziki wa Injili.
Leo katika toleo hili maalum, Ijumaa linawakumbusha wasanii hao walioaga dunia na namna vifo vyao vilivyotokea.

ALBERT MANGWEHA ‘NGEA’
Alikuwa msanii wa Bongo Fleva. Akiwa na miaka 31 alifariki dunia Mei 28, 2013 nchini Afrika Kusini. Chanzo cha kifo chake inadaiwa ni matumizi yaliyopitiliza ya madawa ya kulevya. Alizikwa Morogoro, Tanzania, Juni 6, 2013.

LANGA KILEO ‘RAIS WA GHETO’
Alikuwa msanii wa Bongo Fleva. Alifariki dunia Juni 13, 2013 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar akiwa na miaka 28. Kifo chake kilithibitishwa kuwa, kilitokana na kuzidiwa na Ugonjwa wa Malaria. Alizikwa Juni 17, kwenye Makaburi ya Kinondoni, Dar.

MUHIDIN GURUMO ‘MAALIM’
Alikuwa mkongwe wa muziki wa dansi Bongo. Mpaka kifo chake kilichotokea Aprili 13, mwaka huu kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili akiwa na miaka 74, alikuwa mwanamuziki wa Msondo Music Band. Kifo chake kilisababishwa na kusumbuliwa na matatizo ya moyo. Alizikwa Aprili 15 kwenye Makaburi ya Kijiji cha Masaki, Kisarawe, Pwani.

FATUMA BINTI BARAKA ‘BI KIDUDE’
Alikuwa mwanamuziki wa taarab. Alifariki dunia Aprili 17 2013 Bububu mjini Zanzibar akiwa na miaka inayodaiwa haipungui mia moja. Alizikwa siku iliyofuata, kwenye Makaburi ya Bububu, Zanzibar.

SHEM IBRAHIM KALENGA
Alikuwa mwanamuziki wa dansi. Alifariki dunia Desemba 15, mwaka huu kwenye Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam akiwa na miaka 64. Haijathibitishwa ugonjwa uliomuua. Alizikwa Desemba 16 kwenye Makaburi ya Kisutu, Dar.

MWANAISHA MOHAMED MBEGU ‘AISHA MADINDA’ENZI ZA UHAI WAKE.

MWANAISHA MOHAMED MBEGU ‘AISHA MADINDA’
Alitikisa kwenye eneo la unenguaji kwenye bendi ya muziki wa dansi. Alifariki dunia Desemba 17, mwaka huu Mwananyamala, Dar es Salaam akidaiwa kuchomwa sindano yenye madawa ya kulevya kiasi cha kuwa sumu kali mwilini. Alizikwa Desemba 19 kwenye Makaburi ya Kigamboni jijini Dar. Mpaka kifo chake alikuwa na miaka 35.

SUDI MOHAMED ‘MCD’
Alikuwa mpiga tumba kwenye Bendi ya The Afrcan Stars ‘Twanga Pepeta’. Alifariki dunia Januari 27, mwaka huu mjini Moshi akisumbuliwa na matatizo ya kifua. Alizikwa Januari 28, mwaka huu kwenye Makaburi ya Njoro, Mjini Moshi.

HAMIS KAYUMBU ‘AMIGOLAS’
Alikuwa mwimbaji wa zamani wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’. Alifariki dunia Novemba 9, 2014 kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa siku kadhaa akisumbuliwa na matatizo ya moyo. Alizikwa Novemba 10, kwenye Makaburi ya Kisutu jijini Dar.

Steven Kanumba enzi za uhai wake.

STEVEN KANUMBA
Alikuwa msanii nyota wa filamu za Bongo. Alifariki dunia Aprili 7, 2012, Sinza jijini Dar baada ya kuangukia sehemu ya nyuma ya kisogo. Mpaka anaaga dunia, Kanumba alikuwa na miaka 28. Alizikwa Aprili 10, kwenye Makaburi ya Kinondoni, Dar akiwa na miaka 28.

MARIAM KHAMIS ‘PAKA MAPEPE’
Alikuwa mwanamuziki wa taarab wa Bendi ya Tanzania One Theatre ‘TOT’. Alifariki dunia Novemba 13, 2012 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar kwa matatizo ya uzazi wakati akijifungua. Alizikwa Novemba 14 kwenye makaburi ya Magomeni, Dar.

GEORGE OTIENO ‘TYSON’
Alikuwa msanii na mwongozaji wa filamu za Bongo. Alifariki dunia Mei 31, mwaka huu kwa ajali ya gari mkoani Morogoro akiwa na miaka 31. Alizikwa Juni 14, Kijiji cha Siaya, Kenya.

AMINA NGALUMA ‘JAPANESE’
Anaitwa Amina Ngaluma. Alikuwa mwimbaji wa bendi mbalimbali nchini ikiwamo Double M Sound na African Revolution. Alifariki dunia Mei 15, mwaka huu nchini Thailand baada ya kupatwa na uvimbe kichwani. Alizikwa jijini Dar, Mei 24, 2014 kwenye Makaburi ya Tabata, Dar.

ADAM KUAMBIANA
Alikuwa msanii wa sinema za Bongo. Alifariki dunia Mei 17, mwaka huu, Sinza jijini Dar baada ya kuugua ghafla. Alizikwa Mei 20, kwenye Makaburi ya Kinondoni, Dar akiwa na miaka 38.

RECHO HAULE
Alikuwa msanii wa filamu Bongo. Alifariki dunia Mei 27, mwaka huu kwenye Hospitali ya Lugalo jijini Dar kwa matatizo ya uzazi wakati wa kujifungua akiwa na miaka 26. Alizikwa Mei 30 kwenye Makaburi ya Kisutu, Dar.

Zuhura Maftah 'Merisa'.

ZUHURA MAFTAH ‘MELISA’
Zuhura Maftah ‘Melisa’ (39) alikuwa chipukizi wa Bongo Muvi. Alifariki dunia Septemba 8, 2013 katika Hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar baada ya kusumbuliwa na uvimbe kichwani. Alizikwa kwenye Makaburi ya Kinondoni, Dar.

MZEE MANENTO
Mzee Manento (73) alikuwa msanii wa Bongo Movies. Alifariki dunia Oktoba 29, 2014 katika Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni, Dar baada ya kusumbuliwa na maradhi ya moyo kwa muda mrefu. Alizikwa kijijini kwake, Mamba-Miamba wilayani Same, Kilimanjaro.

JUMA KILOWOKO ‘SAJUKI’
Sajuki (26) alikuwa staa mkubwa wa sinema za Kibongo. Alifariki dunia Januari 1, 2013 katika Hospitali ya Muhimbili, Dar baada ya kusumbuliwa na maradhi ya uvimbe na kansa ya ini. Alizikwa kwenye Makaburi ya Kisutu, Dar.

SAID NGAMBA ‘MZEE SMALL’
Mzee Small (59) alikuwa mkongwe wa vichekesho Bongo. Alifariki dunia Juni 8, 2014 katika Hospitali ya Muhimbili, Dar baada ya kusumbuliwa na kiharusi kwa muda mrefu. Alizikwa kwenye makaburi ya Tabata-Segerea, Dar.

YESAYA AMBIKILE ‘YP’
YP (26) alikuwa msanii wa Bongo Fleva kutoka Kundi la TMK Wanaume Family. Alifariki dunia Oktoba 20, 2014 kwenye Hospitali ya Temeke, Dar baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kifua kwa muda mrefu. Alizikwa kwenye makaburi ya Chang’ombe, Dar.

AHMED ALLY UPETE ‘GEEZE MABOVU’ ENZI ZA UHAI WAKE.

AHMED ALLY UPETE ‘GEEZE MABOVU’
Geeze Mabovu alikuwa msanii wa Bongo Fleva. Alifariki dunia Novemba 12, 2014 baada ya kuumwa kwa zaidi ya mwaka mmoja. Alizikwa huko Iringa katika makaburi ya Makanyagio.

JOHN STEFANO MAGANGA
Alikuwa mwigizaji wa sinema za Kibongo. Alifariki dunia Novemba 24, 2012 katika Hospitali ya Muhimbili, Dar baada ya kuugua ghafla. Alizikwa kwenye makaburi ya Kinondoni, Dar.

JAJI KHAMIS ‘KASHI’
Mwigizaji Kashi alifariki dunia Juni 10, 2013 katika Hospitali ya Muhimbili, Dar alikokimbizwa baada ya kuzidiwa ghafla. Alizikwa kwenye makaburi ya Kinondoni, Dar.

RAMADHAN MKIETY ‘SHARO MILIONEA’
Sharo alikuwa ni staa wa vichekesho na Bongo Fleva. Alifariki dunia Novemba 26, 2012 baada ya kupata ajali mbaya huko Muheza, Tanga. Alizikwa kijijini kwao, Lusanga, Muheza mkoani Tanga.

MAREHEMU SHERRY MAGALI ENZI ZA UHAI WAKE.

SHERRY MAGALI
Sherry alikuwa mchekeshaji na mwigizaji wa sinema za Kibongo. Alifariki dunia Oktoba 21, 2014 kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro baada ya kuugua kifua kwa muda mrefu. Alizikwa kwenye Makaburi ya Mji Mpya, Morogoro.

Wakati huohuo, taarifa zilizotufikia zinasema kuwa, yule mchungaji aliyewahi kutabiri vifo vya wasanii wawili wa filamu na Bongo Fleva ameibuka tena na kutabiri kuwa, jinamizi la vifo vya wasanii bado lipo ambapo amesema:

“Natabiri tena vifo vya wasanii nchini. Kwamba, hadi kufikia Februari mwakani (2015), wasanii wawili watapoteza maisha.
“Lakini ili kukwepa mauti wasimame katika roho wakimwomba sana Mungu na kutoa sadaka bila kusahau kuwasaidia yatima na wazee.” Naye mtabiri maafuru nchini, Maalim Hassan Hussein Yahya amesema roho ya mauti kwa wasanii ipo inazunguka, itafanya kazi hiyo kufikia Aprili mwakani.
Global Publishers, wachapishaji wa Magazeti Pendwa ya Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Uwazi, Amani, Risasi Mchanganyiko na Risasi Jumamosi tunasema; R.I.P wasanii wetu!

RAY C ANG’ATWA NA PAKA KUFA NDANI YA SIKU 97!


Staa anayetamba na ngoma mpya ya ‘Nshumu nshumu’, Rehema Chalamila ‘Ray C’ hivi k aribuni alijikuta katika wakati ngumu baada ya kuvamiwa na paka na kumng'ata kwenye mguu.Sosi wa habari hii alisema kuwa Paka yule alikuwa eneo la Methadone Mwananyamala Hospitali ambapo mwanamuziki huyo anakunywa dawa.Staa anayetamba na ngoma mpya ya ‘Nshumu nshumu’, Rehema Chalamila ‘Ray C’.

“Alipopita Ray C alirukiwa na paka na kumgangania mguu alijaribu kumzuia lakini hakufanikiwa kitendo kilichozua utata kwani bila watu kumsaidia paka yule asingetoka mguuni kwake”, alisema Sosi.
Aidha Sosi huyo alisema kuwa baada ya paka huyo kumvamia mambo yake yamekuwa magumu ni mtu ambaye anaomba hata mia tano na kwa sasa amefunga mghahawa wake.

“ Yaani Ray C kwa sasa anatia aibu kwani maisha yamemharibikia mpaka watu wanadai kuwa huenda yule paka hakuwa wa heri, amekuwa mlevi anavuta sigara ovyo mpaka mwenye nyumba wake hamtaki tena nadhani mkataba wake umesitishwa”, alisema Sosi.

Baada ya habari hizi kutua kwenye meza ya Ijumaa mwandishi alimwendea hewani Ray C ambaye alikiri kuvamiwa na paka na kudai kuwa yeye haamini kama unaweza kuwa ni uchawi anahisi alimkanyaga mkia bila kujua.

“Yaani watu wanapenda kuongea sana mimi kwa sasa mambo yangu yanaenda vizuri tu si mnaona hata nyimbo nimetoa, paka ni sihu ya siku nyingi mpaka nishapona jeraha, duka nimefunga kwasababu nataka kufungua duka kubwa la nguo na nusu yake nitafungua ofisi nyingine, ” alisema Ray C Aidha Ray C alipinga vikali suala la kuvuta sigara na kudai kuwa watu wanaompakazia wana nia ya kumharibia mambo yake kwasababu kwa sasa wameona ana maendeleo.

SHOO YA DIAMOND DAR LIVE YAACHA HISTORIA, chek hapa

Mwanamuziki Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' akipozi katika picha na mashabiki baada ya shoo ya nguvu Dar Live.

Diamond akiwa na tuzo pamoja na cheti baada ya kuibuka mshindi wa shindano la Ijumaa Sexiest Bachelor.

Diamond Platnumz akifanya makamuzi ya hatari Dar Live.

Diamond akifanya yake stejini.

Diamond akicheza na dansa wake.

Baada ya Gemu kubuma, Msanii 20% Anaswa kwa Sangoma….!!



Makubwa! Kichwa cha Bongo Fleva kutoka pande za Kimanzichana mkoani Pwani, Abas Kinzasa ‘20%’, anadaiwa kunaswa laivu akiwa kwa mganga wa kienyeji akipata tiba ya kupunguza na kuondoa sumu ya utumiaji wa bangi na pombe, Ijumaa Wikienda lina ‘pakeji’ kamili.




Abas Kinzasa ‘20%’.



Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, ishu hiyo ilijiri katika Kijiji cha Ngukumo mkoani Tabora baada ya mameneja wa wasanii wa Bongo Fleva, Papa Misifa na Steve Mbaga kumshika mkono 20% na kutafuta mganga wa kienyeji ambaye aliwatangazia kuwa ana dawa zinazoweza kumuondoa sumu hiyo.



Baada ya kunyetishiwa stori hiyo, gazeti hili liliwatafuta mameneja hao ambao walisema walilazimika kufanya hivyo ili waweze kumrudisha 20% kwenye gemu kwa mara nyingine kwani bado wanaamini ana uwezo mkubwa kwenye muziki wa Bongo Fleva.



“Kiukweli mimi na mwenzangu tumekuwa tukisikitishwa kwa muda mrefu baada ya 20% kubobea kwenye matumizi ya pombe na bangi na hasa alipozidiwa hadi akashindwa kufanya muziki huu ambao tunaamini kwake ndiyo ilikuwa ajira pekee.




“Kwa kutambua hilo tulimtafuta na kuongea naye, alipokubaliana nasi tukaamua kumpeleka kwa mganga wa kienyeji, ameshapata tiba na tayari ameonyesha kujitambua, hivyo hivi karibuni tunaanza kufanya naye kazi na ndiyo tunatoka kumlipia nyumba ya kuishi maeneo ya Mwananyamala Hospitali,” alisema Papa Misifa.



Ijumaa Wikienda lilimtafuta 20% ambaye mwaka 2011 alichukua tuzo tano za Kili na kumuuliza juu ya suala hilo ambapo alikuwa na haya ya kusema: “Ni kweli Papa Misifa na Steve Mbaga wamejitahidi sana kunifanya niachane kabisa na matumizi ya pombe maana walinipeleka kwa mganga wao ambaye kweli amenisaidia. “Ujue kilichokuwa kikiniyumbisha siku zote hizo ilikuwa ni pombe maana bangi ilikuwa si kiivyo, nilipokuwa nakunywa pombe kweli ilikuwa ikinitoa kwenye njia na kunifanya kujiona mimi ndiyo mimi kiasi cha kushindwa hata kuwaheshimu wenzangu na ndiyo jambo pekee ninaloweza kusema limenifanya kuwa hivi. chanzo bofya hapa nothing new

Wanasayansi wa kampuni ya Google: Wabuni magari yasiyotumia dereva, Click hapa usome sifa zake






Inawezekana kuwa na magari yasiyokuwa na dereva? Kampuni ya mawasiliano ya kompyuta ya Google inasema ndiyo. Magari hayo yapo na yataongozwa kwa kutumia kompyuta pekee, huku yakiwa na uwezo mkubwa wa kuepuka au kutosababisha ajali barabarani.


Wanasayansi wa Google wanaosimamia teknolojia hiyo mpya, wanaamini kwamba madereva wanafanya makosa mengi wawapo barabarani, yakiwepo ya kizembe ama bahati mbaya na ndiyo yanakuwa chanzo cha ajali mbaya barabarani.


Wakati teknolojia ya kompyuta ilipogundulika, wanasayansi walisema wamegundua mbinu ya kufuta makosa ya kibinadamu katika shughuli za hesabu.


Waliamini kuwa kila hesabu 500 afanyazo mtu ambaye ni mtaalamu wa fani hiyo, lazima kuwepo na makosa yasiyopungua mawili. Lakini baada ya kugundua kompyuta, maelfu kwa maelfu ya hesabu yanaweza kufanyika bila makosa.


Makosa hayo ya kibinadamu yanayoweza kufanywa na mtu bila kukusudia, ndiyo yanayoaminika kuweza kufanywa na dereva yeyote akiwa barabarani.


Magari hayo yako je?


Mtaalamu wa kompyuta katika Chuo Kikuu cha Stanford, Profesa Sebastian Thrun, anayesimamia, teknolojia hiyo akisaidiana na mhandisi wa kampuni ya Google, Chris Urmson, wanasema teknolojia hiyo itasaidia kuepusha ajali, foleni na pia kupunguza kiwango cha mafuta yanayopotea kutokana na uendeshaji usiofaa.


Mhandisi Urmson anasema magari hayo hayatakuwa na tofauti kwa kiasi kikubwa na mwonekano au miundo ya magari yaliyopo sasa. Kama haitoshi yana chaguo la ama liendeshwe kwa kompyuta ama na dereva.


Mwonekano wake


Kimwonekano, magari hayo anayaelezea yatatofautiana na mengine, kwa kuwa na kifaa maalumu juu ambacho kinasaidia mawasiliano na kutambua maeneo.


Anasema kwenye mfumo wa kompyuta zitatumika programu mbalimbali kama vile ya 3D, ambayo itasaidia kuliongoza gari kulingana na ramani ya eneo. “Hii ina maana kwamba magari yote yatakuwa yanatumia ramani ambayo lazima iingizwe kwenye mfumo wake ili itambue barabara itakazopita ili kufika aneo ambalo mhusika ama wahusika wanataka

UNAFAHAMU KUWA GOOGLE INATUMIA KIVINJARI KUTUNZA HISTORIA YA MAISHA YAKO YA KILA SIKU? SOMA HAPA

 

Hebu jibu haraka-haraka! Ulikuwa wapi Jumanne iliyopita majira ya saa 12:35 jioni? jibu lako huenda likawa hivi “Mimi… sina kumbukumbu iwayo yoyote ile.


Kwa kweli akili za watu wengi hazitendi kazi kwa mfumo huo. Lakini uwezekano mkubwa ni kwamba, Google wanafahamu ulipokuwa. Bila shaka wanafahamu mahali ulipokuwa siku nyingine nyingi, vilevile. Nao wanao uwezo kabisa kukufahamisha, wakikuruhusu kuyaishi mapito yako upya hatua moja baada ya nyingine.


Kama unatembea na kifaa chochote kiendeshwacho na Google (kama vile simu aina ya Android au tabiti (tablet)), basi kulikuwa na swali wakati wa kukiunganisha kifaa hicho endapo ungependa Google itoe taarifa kwa mitambo yake mikuu kwamba upo mahali gani. Hii ndiyo habari.


Unajua ni kwa jinsi gani Google sasa inao uwezo wa kimazingaombwe wa kufahamu ni wapi ufanyapo kazi na kukutahadharisha juu ya misongamano ya magari katika barabara unayoitumia? Hiyo taarifa uliyoiruhusu mwanzoni wakati ukiunganisha kifaa chako ndiyo inayowezesha jambo hili.


.Anglizo : kama umekuwa ukifuatilia kwa makini, huenda ulishaliona hili huko nyuma. Si jambo geni. Kwa kweli, limekuwepo kwa miaka kadhaa. Hata hivyo, Greg Kumparak anaeleza kuwa ilikuwa wakati murua kabisa kubaini watu wengi tu ambao walilifahamu hili, hata alipowahoji marafiki zake ambao wao wamekaa kiteknolojia zaidi. Hivyo basi, chukulia hili kama tangazo lenye kustusha kwa manufaa ya umma.


Kwa kweli ni jambo la kushtua, katika viwango vyake; linawafanya watu kufikiria ni kiwango kikubwa kiasi gani cha habari wanazozikusanya Google. Lakini habari yoyote iliyopo pale, iko pale kwa sababu wewe uliwapa dole gumba la ndiyo wakati fulani, hata kama ilikuwa ni kwa kutokutafakari, wewe ukabonyeza vitu fulani wakati unakiunganisha kifaa chako kipya.


Endapo kwa ghafla sasa unaanza kutambua kwamba kuna mahali fulani hivi ulikuwa unapatembelea ambako usingependa pawepo katika historia yako (mimi simhukumu mtu hapa jamani), basi unaweza ukafuta kumbukumbu hiyo siku-kwa-siku ama kuifuta kumbukumbu yako yote ya wapi ulikuwa kwa ujumla wake kwa mkumbo mmoja.


Google walizindua mfumo wa kwanza wa kifaa hiki kipindi kile kile walipoanzisha programu tumishi ya Latitude. Baada ya kuondoa Latitude, waliiacha kivinjari chake, wakiinakshi na kuiongezea umaridadi fulani-fulani kadri muda ulivyosonga. Mbinu mojawapo iliyo poa sana: pitisha kielekezaji (mouse) chako chini ya grafu (jedwali) pale chini yake. Ramani itakayojitokeza juu yake itaonyesha mapito yako ya siku nzima, kutoka mahali hapa ulipokuwa hadi mahali pengine ulipokwenda.


Greg Kumparak anasema yeye alitumia saa moja hivi na ziada, nakisha upya tena mwezi mmoja uliopita wa maisha yake,akijaribu kukumbuka kila kituo kilikuwa kwa makusudi yapi. Oh, na ile grafu (jedwali) Yenyewe inanakili umbali uliotembea ukishabihiana na muda uliotumika kutoka pale ulipoianza siku yako (hivyo, kwa walio wengi, ni kuanzia nyumbani kwako), yote hii ni pamoja na jumla ya umbali uliotembea kila siku.
Chanzo:Techcrunch.com

KIKOSI CHA YANGA KILICHO CHAPWA NA SIMBA 3-1

1.Juma Kaseja - 29
2.Mbuyu Twite - 6
3.David Luhende - 3
4.Nadir Haroub "Cannavaro" - 23(C)
5.Kelvin Yondani "Cotton" - 5
6. Athuman Idd " Chuji" - 24
7.Mrisho Ngassa - 17
8.Frank Domayo - 18
9.Didier Kavumbagu - 7
10.Hamis Kiiza - 20
11.Haruna Niyonzima - 8
Subs:
1.Deogratius Munishi "Dida" -30
2.Juma Abdul - 12
3.Oscar Joshua - 4
4.Rajab Zahir - 14
5.Reliants Lusajo - 9
6.Nizar Khalfani - 16
7.Saimon Msuva
8. Hassan Dilunga - 26
9.Jerson Tegete - 10
10.Emmanuel Okwi - 25
11. Said Bahanuzi - 11
12.Hamis Thabit - 22
Older Posts
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top