WAKUBWA TU! NAMNA YA KULINDA NDOA

1. Wakati ukizungumza nae, jaribu kuzungumzia "hisia" kama vile kumbu kumbu yako ya utotoni, matarajio ya baadae au matamanio yake. Mada hii ya mazungumzo yenu yatafungua milango ya hisia zake ghafla.

2. Wanawake huhitaji mwanaume asiyekuwa na uoga wa kuwamiriki na kuwaongoza. Wakati unazungumza na mwanamke tawala mazungumzo yenu na kamwe usimpe nafasi ya yeye kuanza kufikiri kuwa nini ulichokuwa ukizungumzia.

3. Kuwa makini wakati unapokuwa ukizungumza nae huku akikupatia majibu yasiyo na hisia zozote za mapenzi. Hapo utajua kunakitu, hivyo kama kwa bahati mbaya uko nae karibu kiasi cha kugusana, basi jisogeze pembeni wakati ukiwa unaendelea kuongea ili asishtukie au unaweza kumuona hayuko sawa katika utoaji majibu.. kwa kawaida atakuonyesha ishara, hivyo kuwa nazo makini.

4. Kumbuka hii kauli mbiu "Ucheshi/vituko si mapenzi". Wanawake huvutiwa sana na wanaume wanaoweza kuwafanya wawe na furaha muda wote. Usijikite zaidi katika kufanya utani unaopita kiasi na kusahau ulichokuwa unaongea. Bali jikite zaidi katika mambo yanayomfanya ajisikie kuwa na msisimko na starehe wakati ukonae.

5. Zama katika undani wa mazungumzo baina yako na yeye. Mwanamke huendana na mwanaume asiyekuwa muoga wa kuzungumzia mambo binafsi kwa ukaribu.

6. Wanawake wengi hupenda kujua maoni yako kuhusiana na jinsi unavyomuona. Mwambie vitu unavyoviona kutoka kwake, lakini jaribu kuwa makini ili usitamke vitu vingine vitakavyo msababishia apoteze furaha.

7. Epuka kumpa ofa nyingi mwanamke, mwanamke huwa na mashaka na mwanaume anayempatia vitu vingi kwa wakati mmoja ama kila mara. Kwasababu atafikiri vitu unavyompatia ni kutaka kumvutia tu ili umpate kiurahisi. Kitu ambacho baadae kitaleta madhara makubwa.

8. Kama unahitaji kujua njia nzuri ya kuweza kuongea na mwanamke au msichana bila kumfanya asikudharau au kuboreka, basi usitumie njia ya kumuuliza maswali mengi katika mazungumzo yenu. Bali jaribu kueleza mawazo yako kuhusu vitu flani.

9. Kumbuka kauli juu ya kuuliza maswali: Badala ya kumuuliza "wewe umekulia wapi?", uliza "unaonekana kama hujakulia maeneo haya!" Hii itakusaidia wewe kufanya uchunguzi juu yake bila yeye kujua.

10. Usifiche utambulisho wako - zungumza vitu kutoka katika hisia zako, onyesha uhalisia wako katika kuzungumza na usitumie mikogo ya mtu yeyote.

Njia bora ya kufikiria jinsi ya kuzungumza na mwanamke, ni kutambua njia sahihi ya mazungumzo ya furaha na yakimahaba utakayopenda kuitumia, isipokuwa usimuige mtu. Kuzungumza na mwanamke sii vigumu bali nikujua ni vitu gani hasa mwanamke hapendi kuvizungumzia na vitu gani anapenda kuvisikia. Fuata maelekezo hapo juu utaona matunda yake...kisha rudi toa maoni yako hapa.

MUHIMU: Maelekezo haya yote yatafanikiwa kwa mwanamke mwenye kuhitaji mapenzi ya kweli - yani sio kwa wanawake wanaolenga kuchota pesa kwako na kutokomea. Hivyo kuwa makini sana

HAKUNA HOBI YA NGONO, UGONJWA SOMA UPATE SURUHISHI



MARA kadhaa utakuwa umekutana na marafiki wanaozungumza maneno mengi kuhusu ngono. Baadhi wanapozungumza, wanaonyesha wazi kutopendezwa na hali yao ya kupenda ngono kupita kiasi, lakini wengine huongea kwa kujisifu kwa vile ni mahodari wa kushiriki tendo lile.

Wanaojisifu, ndiyo hawa huja na kauli kuwa wao hobi yao ni mapenzi. Neno hili, hobi, ni la kiingereza linalomaanisha kitu ambacho mtu anakipenda. Mtu atasema hobi yake ni kusoma, mwingine michezo au muziki na kadhalika. Kila mmoja anacho akipendacho, yaani akikipata hicho, roho yake inakuwa raha burudani.

Katika siku za hivi karibuni nimeshuhudia mastaa wawili wakizungumzia ngono, ambao ni Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Baby Madaha. Lulu alisema ngono zimekuwa zikimtesa kiasi kwamba kila mara hujikuta katika hali ya kutaka kufanya mapenzi, kitu ambacho mwenyewe anaamini ana jini mahaba.

Kwa upande wake, Baby Madaha yeye anakuja live kabisa akidai kwamba, kwake yeye, kufanya mapenzi ni hobi yake, yaani ndicho kitu anachokipenda kuliko vitu vingine vyote duniani, yaani kwake yeye, kushiriki tendo akiwa na mwenzi wake ndo faraja yake.

Wazungu wana msemo wao mmoja maarufu unaosema too much of anything is harmful, kwa tafsiri isiyo rasmi ni kwamba kitu chochote ukikizidisha, kitakupatia madhara.

Kushiriki tendo la ndoa ni kitu kinachofurahiwa na wengi, wake kwa waume, ingawa kila mmoja ana aina ya ufurahiaji wake. Wapo wanaozidisha ufanyaji wa tendo hili kutokana na sababu mbalimbali. Kuna wanaofanya hivi ili kujipatia kipato. Anakesha usiku kucha akibadilisha wanaume kwa ajili ya kipato.

Lakini wapo ambao wanapenda kushiriki tendo kwa sababu ya raha tu na siyo kingine. Kwa wote wenye aina hii ya mahitaji, wanaambiwa kuwa wana pepo la ngono!Sisemi kuhusu machangudoa, kwa sababu wote tunajua kuwa hawa wanafanya hivi ili kupata hela, nazungumza na wanawake na wanaume ambao muda wote wanawaza ngono na hata wakifanya hawaridhiki. Anatoka kuchepuka sehemu, lakini anapopanda kwenye daladala macho yake yanavutiwa na mwanamke mwingine na yupo tayari kumtongoza na kulazimisha kwenda naye muda uleule.

Ukimuona mtu wa aina hii, ni wa kumsaidia kwa sababu huo ni ugonjwa. Binadamu anao uwezo mkubwa wa kuhimili hisia za mapenzi yake. Wale waliooa au kuolewa wanaweza kuwa mashahidi wazuri wa hili. Unaweza kukuta wanandoa wanakaa hata wiki mbili bila kukutana, ingawa wanalala kitanda kimoja.

Tendo la ndoa ni kitu cha afya. Mwili hujiweka vizuri zaidi kwa ushiriki wake, lakini unapozidisha dozi, ni tatizo. Ugonjwa huu unatibika, nenda hospitali, onana na daktari bingwa wa saikolojia, atakueleza kwa nini unakuwa hivyo ulivyo na nini suluhisho la kudumu. by GP

Ukitaka kujua Mke siyo ndugu yako soma hii hapa upate undani.

 



Jamaa karudi kazini mpole!

MKE : vipi leo mbona mapema na uko mpole sana, kuna nini?
MUME : ofisi yetu imeungua na watu wote wamekufa ,
MKE : ilikuwaje wewe ukapona?
MUME : nilikuwa chooni , jirani na ofisi najisaidia .
MKE : Loh, masikini! Familia zao itakuwaje ?
MUME : watalipwa milioni 113 kila mfiwa .
MKE KWA HASIRA : ona sasa na wewe kunya kunya kwako umetukosesha hela za bure hizo!

Amwacha mumewe na dadake uchi barabarani


Mwanamke kwa jina Ting Su nchini Uchina alimwacha mumewe na dadake bila nguo barabarani baada ya kuwapata wakifanya mapenzi Ting Ting Su aligundua kwamba mumewe alikuwa akimdanganya na dadaake na kuwafuata hadi katika kituo kimocha cha maduka akitumia teknologia katika simu yake ambapo aliwapata wakichemshana katika gari la mumewe.

Wawili hao walitoka ndani ya gari hilo bila nguo kwa kubabaika ili kujaribu kumuelezea kilichokuwa kikendelea lakini waliwachwa na mshangao mkubwa wakati Ting alipoingia ndani ya gari hilo na kuondoka kwa haraka na kuwawacha wawili hao barabarani bila nguo.

Kulingana na gazeti la Metro,shahidi aliyejulikana kama You Meng alisema walioshuhudia kisa hicho walibeba simu zao na kuanza kuchukua picha na yeye hakubakia nyuma.

Mumuwe aligonga dirisha la gari hilo na kumpigia kele mkewe lakini hakujali kamwe aliliondosha gari hilo kwa haraka. BBC

MADAI MAZITO: AUNT ANASA MIMBA NJE YA NDOA, SOMA MCHONGO MZIMA HAPA

Stori: waandishi wetu
Madai mazito! Pamoja na kutumia nguvu kubwa kukanusha kwa miezi kadhaa, bado staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson, anaendelea kugandwa na madai kwamba, amenasa mimba nje ya ndoa, Ijumaa lina mkanda kamili.
Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel akiwa viwanja na shosti yake, Wema Sepetu.
Habari hizo zilishika kasi mithili ya moto wa kifuu baada ya Aunt kunaswa Klabu ya New Maisha iliyopo Masaki jijini Dar, Jumapili iliyopita akiwa ameshiba yaani kitumbo ndi huku akishindwa kukificha baada ya kila kitu kuonekana waziwazi kwa macho yasiyohitaki miwani.
KIGAUNI CHAANIKA KILA KITU
Aunt, akiwa ukumbini humo na mastaa wenzake waliohudhuria kwenye shoo ya msanii wa Bongo Fleva aitwaye Mirrow anayesimamiwa na kampuni ya muigizaji, Wema Isaac Sepetu na Meneja Petit Man, alitinga akiwa amevaa kigauni cha drafti nyeupe na nyeusi ambacho kilionesha vilivyo tumbo lake.
WEMA ADAIWA KUMSINDIKIZA KLINIKI
Kwa mujibu wa mpenda ubuyu wetu ambaye naye alikuwemo ukumbini humo, kwa kumtazama Aunt anaonekana kuwa na ujauzito wa si chini ya miezi minne sasa na kwamba Wema ambaye ni shosti wake anadaiwa kuwa huwa anamsindikiza kliniki lakini staa huyo ameendelea kusisitiza kuwa hana.
UJAUZITO MIEZI MINNE
“Mimi najua muda mrefu na jinsi anavyoonekana kwa sasa hakuna ubishi kwani ujauzito wake una kama miezi minne hivi,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:
Aunt Ezekiel akiwa na dansa wa 'Diamond', Mose Iyobo.
“Mwanamke mjamzito anajulikana kabisa. Hebu mcheki usoni alivyobadilika. Yaani kawa mweupe wakati Aunt huwa ana rangi ya chokuleti. Ukweli ni kwamba ana dalili zote za kubeba mimba.”
MAKE-UP YAMKATAA
Chanzo hicho kilizidi kuweka wazi kwamba, siku hiyo, Aunt hakuwa amechangamka kama alivyozoeleka siku zote na uso wake ulionekana kama mtu aliyechoka na hata ‘make-up’ aliyoweka haikuwa ikionekana vizuri.
NDUGU WAANZA MANENOMANENO
Habari zaidi zilidai kwamba, baadhi ya ndugu na mawifi wa staa huyo wameanza kucharuka wakidai kwamba Aunt atakuwa amepata ujauzito huo nje ya ndoa kwa kuwa muda mrefu hajaonana na mumewe, Sunday Demonte anayedaiwa kuwa gerezani huko Dubai.“Tangu mumewe apate matatizo Dubai hawajaonana hivyo Aunt hawezi kusema ni ya mumewe,” kiliendelea kudai chanzo chetu.
VITABU VYA DINI
Baadhi ya ndugu hao wametaka vitabu vya Dini ya Kiislam viweke wazi kama ni sahihi kwa Aunt kubeba ujauzito nje ya ndoa kwani kwa upande wao wanapinga kitendo hicho na kwamba ni udhalilishaji kwa ndugu yao ambaye alifuata taratibu zote za kumuoa staa huyo.
Aunt Ezekiel wakati wa kufunga ndoa.
MNENGUAJI WA DIAMOND AHUSISHWA
Sosi huyo alidai kwamba ujauzito wa Aunt unahusishwa na mnenguaji wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Moze Iyobo ambaye kwa sasa wamegandana kama kumbikumbi wakisemekana kuwa kwenye mahaba niue.
SHEHE ANASEMAJE?
Ili kuondoa utata huku likijiridhisha kuwa Aunt anakaribia miaka miwili bila kukutana na mumewe, gazeti hili lilizungumza na Shehe Kaima wa jijini Dar ambaye analijua vizuri sakata la staa huyo ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Kwa kawaida mwanamke ambaye hajakutana na mumewe kwa miezi 6 au zaidi baada ya ndoa, hupaswa kwenda mara moja Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata) kulalamika na hatimaye kudai talaka.
“Ikiwa mwanamke ameridhika na hali hiyo, naye akaamua kukaa kimya huku akifanya mambo yake na kuanzisha uhusiano na wanaume wengine maana yake amejitoa mwenyewe kwenye mamlaka ya mumewe, hivyo hapo kunakuwa hakuna ndoa tena.”
AUNT ANASEMA?
Kama alivyojitetea siku ya bethidei yake oktoba, mwaka huu baada ya kuvaa kigauni cha pinki kilichoonesha kitumbo kikianza kuchomoza, katika tukio hilo la Jumapili iliyopita, Aunt ameendelea kusisitiza kuwa ni aina ya magauni anayovaa ndiyo yanayomuonesha na kitumbo lakini hana mimba.
“Sina huo ujauzito, labda ni kwa sababu ya aina ya magauni ninayovaa,” alisema Aunt kwa kifupi.
MIAKA MIWILI ILIYOPITA
Oktoba 18, 2012, Aunt alifunga ndoa na Sunday ambapo mwigizaji huyo alibaki huku mumewe akitimkia Dubai kabla ya baadaye kupata matatizo na kutupwa jela.

DIAMOND: Sitaoa Milele…, unajua kulikon bofya hapa.



Kutoka moyoni? Wakati bimkubwa Wema Isaac Sepetu akijiaminisha na kuhisi kuwa amepata mume ambaye ni baba bora, mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amefunguka kuwa kamwe hafikirii kuoa, Ijumaa lina cha kukuhabarisha.

Kauli hiyo ya Diamond inakuja wiki kadhaa baada ya Wema kuonekana na pete ya ndoa kidoleni kisha kukiri kuvishwa na ‘kichaa’ huyo wa Bongo Fleva ambaye amerejea kutoka Marekani alikotwaa Tuzo ya Msanii Bora wa Kiume Afrika Mashariki zilizokwenda kwa jina la African Muzik Magazine (AFRIMMA) 2014.


Staa Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa kwenye pozi lenye utata.
Hofu ya kuoa

Akizungumza na gazeti hili kwenye mahojiano maalum, Diamond alisema kuwa anahofia kuoa kwa madai kwamba akifanya hivyo anaweza kuanguka kimuziki kitu ambacho hataki kimtokee maishani mwake.

Kumbe!
Jamaa huyo ambaye siku hizi anajiita Dangote (jina la tajiri wa Nigeria, Aliko Dangote) alitiririka kuwa zamani alikuwa na wazo hilo la kuoa lakini akiwatazama wanamuziki wenzake waliooa mwisho wa siku, makali yao hupungua na wengine kupotea kabisa kwenye ramani ya muziki.
Bofya hapa kumsikia Diamond

“Unajua unaweza kuona kama vile nazungumza kitu cha utani lakini ndiyo ukweli wenyewe.
“Kuna wanamuziki wengi walikuwa kwenye peak (kileleni) lakini walipooa tu ‘kiki’ yao ilishuka ghafla katika muziki na wengine wamepotea kabisa.


Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na Mtangazaji wa Radio E-FM, Penniel Mungilwa ‘Penny’.

“Ukifuatilia kwa umakini wapo mastaa wengi duniani ambao umri umekwenda sana lakini hawajaoa. Hata hapa nyumbani kuna mifano hai. Nadhani hofu yao ni kuona kuwa wakifanya hivyo watashuka kimuziki,” alisema Diamond.
Ni kweli kamvisha pete Wema?

Alipoulizwa kama ni kweli amemvisha pete ya uchumba Wema, msanii huyo hakuwa tayari kufafanua kwa kigezo kwamba pete ni urembo kama urembo mwingine kwa mwanamke.
Nje ya boksi

Baada ya kusikia msimamo wa Diamond, gazeti hili lilijiongeza na kutoka nje ya boksi ambapo lilizungumza na baadhi ya wasanii waliooa na wasiooa ambapo walieleza mambo mazito.


Jackline Wolper
Siri yafichuka

Katika mazungumzo yao kwa sharti la kutochorwa gazetini, wasanii hao walidai kwamba Diamond anahofia kupoteza kiki kwa warembo ambao wengi ndiyo mashabiki wake wanaoamini nao wanaweza kupata zali la kuolewa naye ndiyo maana humzingira na kumuomba namba ya simu kila anakokwenda.
Msururu wa mademu

Ilielezwa kwamba kwa kuwa jamaa huyo hupenda kuwa juu ndiyo maana alisharipotiwa kutoka na msururu wa wanawake mastaa ambao huchangia jina lake kuendelea kuwa juu.
Ilidaiwa kwamba wakati anatafuta namna ya kuchomoka kimuziki alidaiwa kutoka kimapenzi na warembo waliokuwa na majina madogo kama Rehema Fabian aliyepata umaarufu kupitia Shindano la Miss Kiswahili.


Jokate Mwegelo.

Ilisemekana kwamba baada ya hapo alidaiwa kuwa na msururu wa wanawake mastaa kama waigizaji Jacqueline Wolper Massawe na Aunt Ezekiel Grayson na Jokate Mwegelo.
Baadaye jamaa huyo alidaiwa kuruka na wasichana ambao hawakuwa na kiki hivyo aliwamwaga ndani ya muda mfupi kama Najma na Natasha.

Baadaye Diamond alitua kwa Wema hadi akafikia hatua ya kumvisha pete ya uchumba mwaka 2012 ndani ya Ukumbi wa New Maisha uliopo Masaki jijini Dar.

Kumbukumbu zinaonesha kwamba muda mfupi baada ya kumvisha Wema pete ya uchumba walimwagana ambapo Diamond alitua kwa Mtangazaji wa Radio E-FM, Penniel Mungilwa ‘Penny’.


Irine Uwoya

Diamond hakudumu na Penny kwa madai kwamba mrembo huyo hakuwa na kiki kama ilivyokuwa kwa Wema ambaye jina lake halijawahi kushuka tangu alipovaa Krauni ya Miss Tanzania 2006/07.
Ilisemekana kwamba hata tuzo zilipungua ndipo akampiga Penny chini na kurudi kwa Wema ambaye inasemekana ndiye anayemng’arisha. Hawa wameoa, je, wameshuka?
Baadhi ya mastaa waliooa ni pamoja na Mohamed Ahmed ‘Z-Anto’, Nurdin Bilal ‘Shetta’, Amini Mwinyimkuu, Lawrence Marima ‘Marlaw’, Amani Temba ‘Mheshimiwa Temba’ na wengineo chanzo: gumzo la jiji

HUYU NDO MCHUMBA MPYA LULU



HAYAWIHAYAWI hatimaye yamekua! Siku chache baada ya sexy lady wa sinema za Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ kutangaza sifa za mwanaume atakayemchumbia, amejitokeza mtu anayetaka kuchukua jumla na si siri tena, Amani limenyetishiwa.



Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’.

SIFA ZAKE
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa familia ya staa huyo anayekimbiza sokoni na filamu yake ya Foolish Age, mchumba huyo anaitwa Johnson lakini ni maarufu kwa jina la JR na pia ni Mkristo kama ilivyo kwa Lulu.

JR ni mfanyabiashara kigogo wa jijini Dar mwenye ‘mahela’ ya kufa mtu.
Pia mchumba huyo ni bosi wa kampuni kubwa ya uandaaji, usambazaji wa kazi za sanaa Bongo.

ALISHAKWENDA KWA AKINA LULU
“Kwa taarifa yenu, tayari JR anafahamika vizuri kwa akina Lulu kwani alishakwenda kujitambulisha na kuna maneno kwamba ndiye aliyempangia nyumba kubwa, Tegeta jijini Dar.

“Unajua yule jamaa aliona fursa akaitumia. Baada ya Lulu kutoka mahabusu kwa matatizo ya kifo cha mwandani wake, Steven Kanumba ndipo JR akafanya juu chini kumnasa hadi akafanikiwa,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:

“Muda siyo mrefu zitasikika cherekochereko za Lulu kuolewa.
“Ukweli ni kwamba hata mama Lulu (Lucresia Karugila) amemkubali yule mchumba kwani ndiye anayemfanya Lulu aonekane kama alivyo kwa sasa.

“Sasa hivi Lulu anaishi kwenye bonge la nyumba kule Tegeta (Dar) na suala la usafiri si ishu. Anabadili tu magari. Kusema kweli kwa sasa bidada mambo yamemwendea vizuri.
“Anachoogopa tu yasitokee kama yale ya Clement wa Wema Sepetu.”

AMANI LASAKA WAHUSIKA
Baada ya kumwagiwa upupu huo, gazeti hili liliwasaka wahusika mmoja baada ya mwingine ili kupata mbivu na mbichi za ishu hiyo.



Mama Lulu, Lucresia Karugila.

MAMA LULU
Kwa kuwa ni jambo la kifamilia, gazeti hili lilipozungumza na mama Lulu, Lucresia Karugila alisema si jambo baya kwa mwanaye kuwa na mchumba hivyo anamkubali (huyo mchumba) huku akiweka wazi kuwa hana kipingamizi chochote.

Alipoulizwa jina la mwanaume huyo na kwamba ni kigogo mwenye fedha nyingi, mzazi huyo alitoa ruksa aulizwe Lulu mwenyewe.

“Mimi sina sababu ya kumkataa mwanaume ambaye wamekubaliana na mwanangu, kikubwa ni makubaliano, namkubali,” alisema mama Lulu.



HUYU HAPA LULU
Kwa upande wake Lulu mambo yalikuwa hivi;
Amani: Mambo vipi Lulu?
Lulu: Poa, naongea na nani?
Amani: (akatajiwa jina la mwandishi) kwanza hongera kwa kupata mchumba.
Lulu: Nani kawaambia?

Amani: Kwa kazi yetu hii hatushindwi kujua. Je, ni kweli umepata mchumba?
Lulu: Ndiyo lakini nisingependa sana kulizungumzia hilo.
Amani: Anaitwa nani?
Lulu: Siwezi kumtaja leo (Jumanne iliyopita). Nitawatajia tu ninyi subirini. Itakuwa surprise (mshangao), siku si nyingi nitamuanika.

Amani: Je, ni kweli ni maarufu kwa jina la JR? Au wewe tutajie hata jina la mwanzo tu.
Lulu: Nimeshasema jamani nitawatajia kwani ninyi mna haraka gani?
Amani: Je, ni kweli ni mmiliki wa kampuni ya burudani? (anatajiwa kampuni).
Lulu: Hayo yote yatafahamika kwenye utambulisho. Naomba niishie hapo ‘coz’ sina cha zaidi kuhusu ishu hiyo jamani subirini siku si nyingi.

MAMA KANUMBA
Baada ya kujiridhisha kuwa sasa Lulu ana mchumba rasmi, ‘kijumbe’ wetu alimfikishia taarifa aliyekuwa mama mkwe wa staa huyo wakati akiwa na Kanumba, mama Kanumba, Flora Mtegoa ili naye atie neno.

Mama Kanumba hakuwa na kipingamizi juu ya suala hilo zaidi ya kuchekelea huku akiweka wazi kuwa Lulu kwa sasa anaweza kuolewa.
“Mimi sina tatizo kabisa, namjua. Lulu anaweza kuolewa na nimempa baraka zote,” alisema mama Kanumba ambaye kwa sasa ni shosti mkubwa wa mama Lulu.

JR SASA
Hata hivyo, gazeti hili halikuishia hapo kwani lilisaka namba ya simu ya kiganjani ya mwanaume huyo ambapo ilipopatikana, alipigiwa, mambo yakawa hivi:
Amani: Habari yako mkuu JR?
JR: Safi, nikusaidie nini?

Amani: Mimi…(akatajiwa jina la mwandishi na kampuni) wewe ndiye JR mmiliki wa kampuni ya…(anatajiwa jina la kampuni).
JR: Kwanza mimi siyo JR ni GR. Huyo JR ni mdogo wangu.
Amani: Mbona sisi tumetajiwa JR ambaye anamiliki kampuni ya…(anatajiwa tena jina la kampuni).
JR: Oke, ndiyo mimi nikusaidie nini?

Amani: Taarifa tulizonazo ni kwamba una uhusiano na Lulu? Yaani wewe ndiye mchumba wake?
JR: Ndiyo, sitaki maswali (tusi na kukata simu).
Tangu kitokee kifo cha Kanumba ambaye alikuwa na uhusiano wa siri na Lulu, bidada huyo hajawahi kuwa na mwanaume hadi huyo mchumba aliyejitokeza.


Chanzohttp://www.gumzolajiji.com

HUYU NDIYE MWANAMKE ANEYEDAIWA KUWA NA MAHUSIANO NA RAIS WA UFARASA

Kashfa hii imetokea wakati Hollande akikabiliwa na kipindi kigumu cha utawala wake

Rais wa Ufaransa François Hollande, ametishia kuwachukulia hatua za kisheria wahariri wa jarida moja nchini humo lililochapisha taarifa za uvumi kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mmoja muigizaji Julie Gayet.

Hollande hakukanusha madai hayo lakini alisema kuwa jarida hilo limekwenda kinyume na maadili ya vyombo vya habari kwa kuingilia maisha yake binafsi.

Jarida hilo, Closer,limechapisha picha kadhaa ambazo linasema zinathibitisha madai kuwa Hollande ana uhusiano wa karibu sana na Bi Gayet.

Bi Gayet mwenye umri wa miaka 41 ni muigizaji msifika wa vipindi vya televisheni.

Duru zinasema kuwa ufichuzi huu umetokea wakati ambapo Hollande anakabiliwa na changamoto kadhaa katika utawala wake, ikiwemo kudorora kwa uchumi jambo ambalo wananchi wanamtarajia kulishuhughulikia.

Inajulikana wazi kuwa bwana Hollande ana mpenzi mmoja tu ambaye ni mwanahabari Valérie Trierweiler.

Hollande pia aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanasiasa mwenzake wa chama cha kisosholidti, Ségolène Royal.

Mwezi Machi mwaka jana aliwasilisha malalamiko yake kwa kiongozi wa mashitaka Jijini Paris, dhidi ya wanablogu na wenye Mitandao ya kijamii kuwa wanaeneza uvumi.
 
Source http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2014/01/140110_hollande_mapenzi.shtml

MSANII WA BONGO ANUSURIKA BAADA YA KUJARIBU KUTOA MIMBA







MSANII nyota wa filamu Tanzania, Salma Jabu maarufu kama Nisha yamemkuta makubwa baada ya habari kuvuja kuwa kumbe sababu ya kuumwa hadi kuzidiwa kitandani, ilitoka na kuchoropoa mimba changa aliyokuwa nayo.

Gazeti la Maskani Bongo lilitonywa na mtu wa karibu wa msanii huyo ambaye yupo ndani ya familia hiyo baada ya kusambaa kwa habari kuwa Nisha aliugua gonjwa la ajabu ghafla katika mitandao ya kijamii na magazeti pendwa.

OBAMA, MICHELLE WADAIWA KUTENGANA


Barack Obama na mkewe Michelle kila mmoja akionekana kuwa kivyake.
Obama akimshika begani Waziri Mkuu wa Denmark, Helle Thorning-Schmidt, wakati wa mazishi ya Mandela nchini Afrika Kusini. Kulia ni Michelle Obama akiwa amenuna.

RAIS wa Marekani, Barack Obama na mkewe Michelle wanadaiwa kutengana. Habari zinadai kuwa wawili hao wanalala katika vyumba tofauti kwa sasa ndani ya Ikulu ya Marekani 'White House'.

Mgogoro baina ya wawili hao ulianza zamani na wameweza kuendelea kuishi pamoja kwa sababu ya watoto wao wawili wa kike Sasha na Malia na kulinda heshima ya urais.

Michelle anadai amechoka na atakutana na mwanasheria wa masuala ya talaka ili aweze kuachana na rais huyo wa 44 nchini Marekani. Michelle ataendela kuishi Ikulu 'White House' kwa muda wote uliobaki katika kipindi cha utawala wa Obama, ila ameweka wazi kuwa watakuwa wakiishi vyumba tofauti.

Anataka kuishi katika chumba kimojawapo cha familia kilichowazi na anajiandaa kuhamisha nguo zake na kila kilicho chake kutoka kwenye jumba lao la kifahari la mamilioni ya dola lililopo Chicago.

Michelle alichanganyikiwa zaidi baada ya Obama kupiga picha za kimahaba akiwa na Waziri Mkuu wa Denmark, Helle Thorning-Schmidt, wakati wa mazishi ya marehemu Nelson Mandela nchini Afrika Kusini.
Obama mwenye miaka 52, alikuwa akifurahi, kunong'enezana na kumshika begani mrembo huyo mwenye umri wa miaka 46 ambaye amekuwa Waziri Mkuu wa Denmark tangu Oktoba 3, 2011.

CHANZO: http://www.nation.com.pk/entertainment/25-Dec-2013/obama-michelle-l...

AUNT EZEKELI ATAMANI KUOKOKA

Licha  ya kubadili dini na kuwa muislam kisha kupewa jina la Rahma, staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel amesema sasa anatamani kurejea ‘ulokoleni’ na kumrudia Yesu kwa kuokoka. 
 
Akizungumza na gpl hivi karibuni nyumbani kwake Mwananyamala jijini Dar, msanii huyo ambaye alibadili dini kutoka ukristo na kuwa muislam baada ya kuolewa na mumewe, Sunday Demonte alisema anajisikia kurudi kwenye ukristo kwa madai ya kumtumikia Mungu kikamilifu.
 
Akionesha msisitizo katika hilo, Aunt alisema moyo wake umekuwa ukitamani kusikiliza mafundisho na mahubiri ya kikristo pamoja na kusikiliza nyimbo mbalimbali za injili.


Wakizungumzia mawazo ya kuokoka ya msanii huyo, baadhi ya mashabiki wake walimshangaa huku wakionesha wasiwasi wake juu ya kusilimu na kudai huenda kubadili kwake dini ilikuwa danganya toto.
 
“Huyu si aseme tu uislam umemshinda? Kasilimu juzijuzi tu hapa na kudai ameanza kusali msikitini, leo anatuambia anatamani kuokoka, hawa mastaa wetu wanamchezea sana Mungu,” alisema Rahma wa Kinondoni jijini Dar.

Huyu Ndiye Queen, Kigoli wa Miaka 21 anayeelezea Patashika anazokutana nazo wakati akitafuta Mwenza wake wa Maisha...!!



Queen ni mtoto wa 4 kati yya familia ya watoto 5. Ni msichana mzuri na mrembo kimtazamo, lakni tatizo kubwa linalomkabili maishani mwake ni nywele ambazo zimekuwa zikimfanya aonekane kama mwanaume…..

Queen amesimulia kuhusu changamoto anazokumbana nazo kutokana na tatizo hilo.
“Nimerithi hizi nywele toka kwa mama yangu na zilinianza nikiwa na miaka 21. Kadri miaka ilivyozidi kusonga mbele, tatizo hili lilizidi kusambaa mwili mzima.
“Mwanzo nilikuwa najisikia vibaya sana maana watu walikuwa wakiniona ni kiumbe wa ajabu, lakini baadae nilizoea na ikanilazimu nikubaliane na ukweli….
Akiongelea kuhusu changamoto za kimahusiano anazozipata ,Queen alikuwa na haya ya kusema:
“Sijabahatika kuwa na mwanaume wa kudumu, wengu hunikimbia kutokana na hali hii”

Mwanamke afanya Mauaji huko simiyu kisa wivu wa mapenzi



JESHI la Polisi mkoani Simiyu linamshikilia mwanamke na mkazi wa Kijiji cha Usiulize wilayani Meatu kwa tuhuma za kumuua mpenzi wake kwa kumvuta korodani, kutokana na wivu wa kimapenzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Charles Mkumbo alisema tukio hilo lilitokea juzi saa tisa usiku katika Kitongoji cha Mlimani Kijiji cha Usiulize Kata ya Mwamalole.

Alisema katika tukio hilo, wapenzi wawili Jumanne Gunda (39), mkazi wa Kijiji cha Kinyambuli wilayani Mkalamo, akiwa amelala na mchumba wake, Mariamu Khamis (49) mkazi wa Kijiji cha Ibaga Wilaya ya Mkalamo mkoani Singida, kulitokea kutoelewana kati yao na kusababisha wagombane.




Katika ugomvi huo, ambao chanzo chake ni wivu wa kimapenzi, Mariamu anatuhumiwa kuzivuta korodani za mpenzi wake na kusababisha mishipa muhimu kukatika na kusababisha kifo cha Jumanne papo hapo.


Kufuatia kifo hicho, Mariamu aliburuza mwili wa mpenzi wake mpaka chooni kwa lengo la kuutumbukiza katika shimo la choo. Hata hivyo kutokana na udogo wa tundu la choo, alishindwa kutumbukiza mwili huo chooni na hivyo kuamua kuutelekeza humo.

Asubuhi kulipopambazuka, majirani wa nyumba waligundua mwili wa marehemu ukiwa umetelekezwa chooni na kutoa taarifa Kituo cha Polisi, ambao walifika katika eneo la tukio na kumtafuta mtuhumiwa, Mariamu.

Baada ya Mariamu kukamatwa, anatuhumiwa kukiri kumuua mpenzi wake katika ugomvi kati yao, uliotokea usiku walipokuwa wamelala wote wawili. Anatuhumiwa kukiri kumvuta korodani zake na kusababisha kifo chake.

"Mkorogo Umenitia Adabu sana"...Wema Sepetu



MISS Tanzania 2006 aliye pia staa wa filamu za Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amevunja ukimya kwa kuweka wazi kuwa, mkorogo umemtia adabu na anajuta kuutumia mwilini mwake.



Wema Sepetu

. Akizungumza juzi na paparazi wetu ofisini kwake jijini Dar, Wema alisema kuwa baada ya kwenda kliniki nchini China na kupata matatibu ya ngozi yake ambayo sasa imerudi kama mwanzo amejifunza kitu.
NI KITU GANI HICHO?
Wema alisema amejifunza kuwa, binadamu anatakiwa kuishi alivyoumbwa na Mungu, mambo ya rangi ya mwili hayana nafasi katika uwezo wa binadamu.
ALIAMINI USTAA NI LAZIMA UWE MWEUPE PEE!
Wema akatoa mpya zaidi aliposema kuwa, uamuzi wake wa kutumia mkorogo ili awe mweupe kama mzungu (yeye ni mweupe) ulitokana na kuamini kwamba, weupe na ustaa ni mambo yanayokwenda pamoja, kumbe sivyo.
“Niliamini weupe sana na ustaa ni Kulwa na Doto, lakini sivyo. Ngozi yangu ya awali ni nzuri, imerudi kama ilivyokuwa, namshukuru sana Mungu,” alisema Wema.
AWAONYA MASTAA WENZAKE
Akiendelea kuzungumza na paparazi, Wema alitoa ujumbe kwa mastaa wenzake wanaotumia mkorogo kuwa, hakuna faida yoyote, kwa sababu mkorogo unaondoa vitamini yote mwilini.
“Daktari kule China aliniambia kuwa licha ya kupoteza vitamini nyingi mwilini, pia mkorogo unakufanya mtu uzeeke kabla ya wakati. Mimi nawaomba kabisa mastaa wenzangu wajiepushe na hii kitu inaitwa mkorogo,” alisema Wema.
ALICHOJIFUNZA KUHUSU KUJIKOBOA
Kujikoboa ni kuwa mweupe sana, lakini Wema anasema alichojifunza kuhusu hali hiyo ni kwamba, ni rahisi sana kuiondoa ngozi ya awali kwa mkorogo lakini inapofika ngozi ya awali inatakiwa kurudi inagharimu sana.
“Ukitaka kuona maajabu sasa, ngozi yako mwenyewe kuibadilisha si kazi na wala si gharama lakini ukitaka irudi kama mwanzo ni lazima ugharimike sana, mimi sitaki tena jamani,” alisema Wema.

DIAMOND AFUNGUKA KWA LULU


STAA kiwango katika tasnia ya filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amekanusha uvumi uliozagaa mitaani kuhusu kutoka kimapenzi na mbabe wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.

Nasibu Abdul ‘Diamond’. Imekuwepo minong’ono ya muda mrefu kitaani kuwa, Diamond analilia penzi la Lulu lakini Diamond au Sukari ya Warembo alipoulizwa kuhusu hilo, alisema siyo kwamba analilia tu bali waliwahi kutoka (haijulikani kwenda wapi) naye, madai yaliyotupiliwa mbali na Lulu.
MADAI YA AWALI
Habari zilizotua katika meza ya Risasi Mchanganyiko zinasema kwamba, wawili hao wanafanya kazi za kisanii pamoja (haikuwekwa wazi ni kazi gani kati ya filamu au muziki) lakini tatizo lililopo kati yao ni Diamond kumtaka Lulu.
Chanzo kilichoomba hifadhi ya jina lake, kilifunguka: “Diamond anashindwa kuelewa, tatizo yeye kila mwanamke anataka kutoka naye. Mwenzake anajua yupo kazini, yeye anataka penzi, ndiyo mzozo uliopo kati yao.”

Wema Sepetu. KAZI KWA DIAMOND
Paparazi wetu alimvutia waya Diamond ili kutaka kupata ufafanuzi kwa upande wake, ambapo aliposomewa maelezo yote alicheka sana kisha akasema: “Nililie penzi la Lulu? Acheni hizo... ngoja nikuambie kitu, siyo kulilia, mimi nimeshawahi kutoka naye. Nilitembea naye kishkaji tu kisha kila mmoja akaendelea na yake.
“Hayo mambo yalishapita na sikutaka kuyaongelea lakini kwa sababu naona kama yanakuzwa, ndiyo maana nimeamua kuweka wazi. Kwa sasa tunaheshimiana kama kaka na dada. Kuna ugumu gani mimi kuwa naye wakati nimeshampitia?”
Risasi: Unasema kweli Diamond?
Diamond: Wa asilimia mia moja.

Penny. Risasi: Una ushahidi gani?
Diamond: Watu wanaojua hii ishu ni wawili tu; Wema (Sepetu) na Penny (Penniel Mungilwa). Niliwaeleza kwa uwazi kabisa hawa ili tusielewane vibaya. Kama huamini waulize. Hawa ndiyo niliowapa siri hii.
Paparazi wetu alijaribu kuwatafuta Penny na Wema kupitia simu zao za mkononi lakini hawakupokea.
TURUDI KWA LULU SASA
Akizungumza kwa sauti ya kujiamini, Lulu alimshangaa Diamond na kusema kwamba, si kutoka naye tu bali hana hata kazi anayofanya naye pamoja.
“Nawashangaa sana eti mimi nifanye kazi na Diamond, kazi gani sasa wakati mimi na yeye tupo kwenye fani tofauti? Muziki na filamu wapi na wapi? Kifupi hayo madai hayana ukweli wowote na kila mtu yupo na yake,” alisema Lulu na kuongeza:


Lulu. “Kwanza mimi siwezi kutoka na Diamond... levo zetu ni tofauti kabisa, wala hazilingani. Mimi nilianza kutoka kabla yake, nimeanza kujulikana toka kitambo hicho nina miaka mitano sijui hata kujifuta kamasi vizuri.... hakuna ukweli wowote.”
TUJIKUMBUSHE
Diamond amekuwa akihusishwa kutoka kimapenzi na mastaa mbalimbali, huku madai hayo yeye mwenyewe akiyakubali, jambo lililosababisha aitwe Sukari ya Warembo.
Mbali na orodha ndefu aliyotoka nayo Diamond, kinachovuta hisia za wengi ni uhusiano wake wa sasa, ambapo haijulikana kama yupo na Penny, Wema au wote kwa wakati mmoja!

MAMBO AMBAYO WANAUME WANAKOSEA WAKATI WA KUTONGOZA MWANAMKE


1.PAPARA
wanaume wengi tumekuwa na haraka sana tunapokuwa tukitaka kuaproach hali inayomfanya mwanamke akuwekee ugumu.mfano umekutana na dada mzuri mmesalimiana hapo hapo unamuomba namba yake.mjomba hata akikupa ujue utasumbuka sana kumpata coz atakufikiria sana juu ya uharaka wako.
2.KUJIFAKE
wanaume wengi tumekuwa tukijipandisha au kujionyesha tofauti na hali zetu.ukiwa unaaproach jaribu kuwa real.huwezi kumwambia mdada unafanya kazi benki afu uko na techno
3.KUTOSOMA MOOD YA MWANAMKE
unapomuaproach mwanamke lazma usome mood yake coz sometime unaweza kutoswa coz hujamsoma mwanamke.unamtongozaje mwanamke asubuhi?,,
4.KUMPONDA UR EX LOVER
mwanamke anakuuliza kwanini uko single,unaanza kumponda ex wako kwa maneno ya kashfa hali kama hii inaweza kumtisha kisaikolojia umtongozae.
5.KULALAMIKA
Unamtongoza mwanamke huku unalalamika juu ya mapenzi oooh mara sijawahi kupendwa.mjomba hapo unaonyesha udhaifu wako.UKITULIA NA KUMTONGOZA MWANAMKE BILA KUYATENDA HAYA MBONA UTAMPATA KILA UMUTAKAE
Older Posts
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top