50 Cent auza nyumba ya vyumba 52

50 Cent

NEW YORK, MAREKANI
RAPA 50 Cent ameshangaza watu kwa kuamua kuuza nyumba yake yenye vyumba 52 kwa thamani ya dola milioni 8.
Msanii huyo wa wimbo wa ‘Candy Shop’, mwaka 2007 alitangaza kuiuza nyumba hiyo kwa kitita cha dola milioni 18.5, lakini sasa ameiuza kwa dola milioni 8, pungufu kwa dola milioni 10.5.
Hata hivyo, thamani ya nyumba hiyo ilionekana kushuka kila mwaka tangu alipotangaza kuiuza mwaka 2007.
Nyumba hiyo mbali ya kuwa na vyumba 52, kuna sehemu ya kiwanja cha mpira wa kikapu, ukumbi wa muziki, Casino na sehemu ya kupaki helikopta.
Msanii huyo kwa sasa amekuwa na wakati mgumu tangu kuuzwa kwa nyumba hiyo kutokana na kupokea lawama za mashabiki wake kwenye mitandao ya kijamii.

TARIME: Mwenyekiti CHADEMA mbaroni Akidaiwa kuiba Mlingoti wa bendera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)



MWENYEKITI wa Chama cha Demkrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Kijiji cha Sokini mji mdogo wa Sirari wilayani Tarime, Denisoni Makanya (44), amepandishwa kizimbani mbele ya Hakimu, Gibogo Wenje, akidaiwa kuiba mlingoti wa bendera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wenye thamani ya Sh 80,000. 


Mwendesha Mashtaka wa Oolisi, George Lutonja, alidai mshtakiwa alitenda kosa hilo usiku Mei 29, mwaka huu. 


Mshitakiwa alikana shitaka na yuko nje kwa dhamana hadi Agosti 4 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.

Shamsa Ford Aonyesha Jeuri kwa Mzazi Mwenzake

 

Staa wa filamu Bongo, Shamsa Ford ameonesha jeuri kwa kueleza kwamba anamlea mwanaye Terry kwa mapenzi tele ili asimkumbuke baba yake, Dickson ambaye wamemwagana. 


Amesema tangu wamwagane na mzazi mwenzake, mtoto wake hajawahi kumuuliza baba yuko wapi kitendo kinachomfanya azidishe mapenzi kwake kwani hata yeye alilelewa na mama yake bila baba. 


“Kama baba yake alikuwa akinipiga mbele yake au kuja akiwa amelewa tilalila unafikiri mtoto atamkumbuka? 

Nimelelewa na mama yangu na sikuwahi kumkumbuka baba mpaka hivi nimekuwa mtu mzima, kwa hiyo sioni shida kumlea mwanangu peke yangu, kila kukicha naongeza upendo kwake,” alisema Shamsa.

AUNT,WEMA SEPETU WAANGUA VILIO BAADA YA KUPATANISHWA

 
Baada ya kula viapo vya kutozikana, wasanii wawili wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Aunt Ezekiel Grayson wamejikuta wakiangua vilio wakati wakipatanishwa na rafiki yao mkubwa ambaye ni pedeshee anayejulikana kwa jina la Daudi Mambya. 




 



Aunt Ezekiel akimbembeleza Wema baada ya kupatanishwa. Habari kutoka kwa shuhuda wetu zilieleza kwamba, tukio hilo lilijiri wikiendi iliyopita kwenye Ufukwe wa Coco jijini Dar ambapo Daudi aliwaita kwa mwaliko wa mishikaki bila wenyewe kujua kinachoendelea.
Habari zilieleza kuwa, Daudi ambaye kwake huwa hawafurukuti, amekuwa akiumizwa mno na tofauti ya wasanii hao kwa sababu ni watu walikuwa wakipendana hivyo kugombana kwao kulikuwa kunaleta shida kwa marafiki zao wengine.
Imefahamika kwamba, Daudi alitumia ujanja wa kuzungumza na kila mmoja kwa wakati wake ambapo alibaini kuwa hakuna aliyekuwa tayari kupatana na mwenzake.
Ilisemekana kuwa, Daudi alitumia ujanja wa kitaalamu ili kila mmoja kumuweka sawa bila kujijua.
“Unajua Daudi ni rafiki yao sana, sasa hakuwa anapendezwa na tatizo ambalo limejitokeza hivyo alitumia njia tofauti ili kuweza kuwakutanisha pamoja tena waweze kupatana,” alieleza mtoa habari huyo.


 



Wakiwa na rafiki yao Daudi Mambya anayedaiwa kuwapatanishwa. Ilielezwa kwamba Daudi alianza kwa kumtafuta Wema na kumpeleka Coco Beach akimuambia kuwa anataka akamnunulie mishikaki huku wakati huohuo akimwambia Aunt naye wakutane ufukweni hapo.Shushushu wetu alizidi kufunguka kuwa Daudi alitangulia Coco na Wema, huku akifanya mawasiliano na Aunt na baada ya muda, Aunt naye aliwasili huku kila mmoja akibaki katika mshangao usioelezeka baada ya kukutana uso kwa uso.
Sosi huyo alisema kuwa Wema na Aunt walipoonana kila mmoja alikuwa kimya lakini Daudi aliamua kuwasomea risala ndefu iliyomwingia kila mmoja.Mambo yakipokaa vizuri, wawili hao walishuhudiwa wakiwa wamekumbatiana huku kila mmoja akiangua kilio kilichochukua takribani nusu saa hivyo kufanya eneo hilo kuwa kama kuna msiba.
“Yaani mpaka Daudi mwenyewe alidondosha machozi baada ya Wema na Aunt kukumbatiana na kuanza kulia.
“Yaani ilikuwa simanzi kubwa sana,” alimalizia shuhuda huyo.Akizungumza na gazeti hili, Daudi alisema kuwa aliamua kuwapatanisha wawili hao kwa kuwa alikuwa hapendezwi na tatizo hilo na kwamba wote ni rafiki zake.


 

Kwa upande wake, Aunt alifunguka ya moyoni:
“Tulipokutana kila mtu alijua tatizo lake na tukaona ni mambo ya kijinga, ikabidi tuweke tofauti pembeni maisha yaendelee.”
Wema alisema: “Mambo ya kugombanagombana hayana msingi na kwa vile ni mtu mzima (Daudi) aliwakutanisha, nikaona yaishe.”Wema na Aunt ambao walikuwa marafiki wakubwa waliingia kwenye mgogoro hivi karibuni baada ya Wema kumtuhumu Aunt kuunga mkono shoo ya Zari All White Party ya mwanadada Zari Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ambaye ni mpenzi wa aliyekuwa mpenzi wa Wema, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Hajui Kama Nimeoa, Penzi Limenoga Nataka Kusema Ukweli Lakini Sujui Nianzie Wapi

Sijawahi kuwa mzinzi tangu nimeoa miaka 5 iliyopita. Hadi hivi karibuni nilipoanzisha uhusiano na binti mmoja..

Tulifahamiana kikazi, yeye yupo idara ya uhasibu. Huja kazini kwangu kila mwisho wa mwezi kwa ajili ya transaction mbalimbali.

Tukazoeana na kuwa wapenzi. Kiukweli mambo yalienda haraka haraka sana na aliingia mazima mazima kiasi kwamba hata kila nilipotaka kumwambia ukweli najikuta nashindwa maana alikua resi ile mbaya.

Ikawa ni mahaba niue, kila tukitoka kazini tupo wote sehemu, weekend tutaenda cinema, beach etc. Yaani ghafla bin vuu anaongelea ndoa. Kila siku ya Mungu lazima agusie ndoa itakua vipi.

Wakati mwingine anaingia Google kusearch magauni ya harusi na viatu na maids wake watavaa nini siku hiyo. yaani nabaki mdomo wazi maana moyoni najua nimeshaoa siku nyingi.

Kila akianzisha hizo story za magauni najitutumua sasa nianze kumwelewesha kwamba nimeoa basi hunikata kauli haraka na kuendelea kusema mambo ya ndoa yetu kwamba napendelea ukumbi gani ndo mzuri.

Sasa tuna miezi miwili ameanza kuongelea suala la kupata mtoto ananiuliza kuwa naonaje akibeba mimba kabisa tufunge ndoa wakati ana mimba. Basi humjibu kuwa tusubiri kwanza asibebe kabisa mimba, nikijibu hivyo anakua mkali anauliza "hiyo mimba unaibeba wewe au mimi?" Mimi nabaki kimya.


Kwa kweli namuonea huruma kwa mawazo aliyonayo, mimi niliingia kwenye huu uhusiano kubadilisha mboga tu and I thought it would be a temporary thing. Kiuchumi yupo vizuri balaa simpati hata kwa dawa.
Ukifika alipopanga thamani za vitu alizonazo ndani ni za gharama sana, na nyumba ni ya kisasa, ana miradi mingi mbali na kazi na alinipeleka anapojenga nyuma ni kama imeisha bado ukuta tu wa nje.

Tatizo pekee ninaloliona ni kuwa huyu binti time is ticking very fast against her age, yupo kwenye mid 30s; somewhere between 30-36 years. Hivyo anadhani amechelewa.

Anasema amepoteza muda mwingi kwenye relationship iliyopita iliyochukua 7 years na jamaa akaoa mtu mwingine na kumuacha yeye, hivyo anasema hataki tena long relationship. Ameshaniunganisha na ndugu kibao. Kila wiki natambulishwa kwa ndugu mpya.

Wakuu, naona huruma Kubreak hii news kuwa nilishaoa. Ingawa nampenda moyoni lakini pia nimechoka maisha ya digi digi ninayoishi maana nikiwa home kwangu usiku lazima anipigie simu na anaongea zaidi ya nusu saa na hapo tumetoka kuonana jioni. Basi najifanya naenda dukani kwa mangi kununua kitu na kupiga stori ili wife asishtuke kuwa naenda kuongea na simu.

I think wengi mnajua maisha ya Ku,cheat yalivyo magumu ni utumwa, ni jela ya nje.

Wakuu nianzeje kumwambia ukweli anielewe? Au nitume mtu mwingine ndo amwambie kama anampa umbea vile?

I need to get out of this mess maana wife somehow ameanza kushtukia mwenendo wangu.

Please, advise

HAKUNA MWANAMKE "USED" KAMA HAFAI KWAKO KUNA MTU KWAKE HUYO MDADA NI MPYA

 
Utamuacha Mwanamke fulani kwa kashfa zote na kejeli za kila namna kwamba hafai na haoleki ILA Mwanaume yule atamchukua na kudate nae na pengine atamuoa na wataishi kwa furaha na kuzaa watoto,atasahau hata kama uliwahi kuwa Boy wake na kashfa zako...Kapata Perfect Match yake....Mwanamke fulani ataachwa na wewe utakutana nae na kumpokea,na pengine utamuoa na kuishi kwa amani. Umepata Perfect match yako..Hii inaitwa Love Circle...

Hakuna Mwanaume wala Mwanamke 2nd hand/Used kwamba hafai...Kama hafai kwako kuna mtu kwake huyo mdada ni Malkia...Kama hafai kwako,kuna mdada anamtamani amfanye awe mfalme wake..

Binadamu hana Mshale wa kuonyesha kilomita ngapi katembea au ana listi ya watu mia ngapi!
Kuna watu wametumika kwelikweli,shusha engine mara 6 na kumwaga oil nyeusi,ila wameolewa na kutulizwa ndani..Wewe unayejiona mpya mpya unanukia Nylon bado unamanga manga...Haijalishi wewe ni Mpya au Used,when ur perfect match arrives, everything else about Past will be history!

By Wastara on Instagram

UMESHAWAHI KUMUONA MCHUMBA YA YOUNG KILLER? ...MUONE HAPA NI NOMA...












Young Killer and his girlfriend, Khalimaty shocked the world by releasing bedroom photos when they were in the 'ACT'



TAZAMA ZARI NA DIAMOND WAKIWA SHOPPING

 

Celebrity couple Zari The Boss Lady and Tanzanian Musician Diamond recently went baby shopping in London in readiness for their bundle of joy that is expected to be welcomed sometime in September this year. 

The baby who is rumoured to be a girl,will be Zari’s fourth child and Diamonds first and the pair seem too excited judging from their posts. 

Diamond who earlier expressed that he could not wait to welcome chibu_juniour was seen trying out various baby strollers and baby cots. 

Here are the Pictures :


Wema Sepetu And Aunty Ezekiel End Their Hostility And Become Friends Again.


Since last week there have been constant news about Wema Sepetu and Aunty Ezekiel's friendship coming to an end. 

Even yesterday some newspapers, and blogs had news of the two celebs swearing not to bury each other when they die. 

But according to reports yesterday evening Wema and Aunty ended their enmity which was growing to dangerous heights. 

One of their close friend called Junaithar arranged a meeting for the two to reconcile and they agreed. They even ate and drink together and these are pics when the two met.



Junaithar is the one who made sure VJ penny and Wema forgot their hostility and became best friends again.

Wastara Amuanika Mbaya Wake..Kumbe Kisa ni Kuolewa na Marehemu Sajuki


Baada ya kipindi kirefu cha tetesi ya staa wa filamu Wastara kuhofia maisha yake, akihisi upo mpango wa kumuangamiza kwa njia mbalimbali ikiwepo ajali, staa huyo amesema tetesi hizo ni kweli na amekwishazitolea ripoti polisi.

Msanii huyo amekiri kupitia eNewz kuwa, ni kweli yupo katika tishio la maisha yake, mhusika mkubwa wa hilo akiwa mwanaume ambaye alikuwa na mahusiano yake wa zamani ambaye hawana maelewano mazuri naye.
Wastara amesema kuwa, amekuwa na historia ya mahusiano mabovu na mtu huyo na kupelekea kuachana naye, na kitendo cha yeye kuolewa na marehemu Sajuki kikiwa sababu ya kuamsha ugomvi upya, na hapa anaeleza mwenyewe mambo yalivyoanza na kujikuta katika hali hiyo na vilevile hatua alizochukua, Wastara.
Wastara amesema kuwa, mwanaume huyo amekwishamtamkia wazi kuwa anahusika na moja ya ajali iliyomkumba, akitumia mambo ambayo ameyaita ya kiswahili kutaka kumuangamiza, jambo ambalo amekwishalitolea ripoti polisi takriban miaka 5 iliyopita.
Staa huyo amesema kuwa, chochote ambacho kitampata kwa mujibu wa maelezo aliyotoa kwa mwanausalama kutokana na vitisho vya bwana huyo, moja kwa moja vitakuwa vimemuweka hatiani, akisisitiza kuwa ana imani kuwa maisha yake yanasonga kwa mipango ya Mungu ambayo mwanadamu hawezi kuvuruga.

Aunty Ezekiel: Sinta Mzika Wema, Familia ya Wema Yacharuka yasema Heri Kajala Kuliko Aunty


‘Nikifa usije kunizika, ukifa sitakuzika’! Ni maneno makali sana kuyatamka kiasi kwamba, enzi za wahenga ilipotokea ndugu, marafiki au majirani wakaapishana kwa maneno hayo, walitafutwa wazee wenye hekima ili kuondoa laana hiyo.

Sasa, hivi karibuni, baada ya kuvunjika kwa urafiki wa ‘kupika na kupakua’ kati ya mashostito wawili walio katika tasnia ya Bongo Movies, Aunt Ezekiel Grayson na Wema Isaac Sepetu maneno hayo yametumika pasipo sababu, Ijumaa Wikienda lina kila kitu!

AUNT BILA KUUMA MANENO

Juzi, Aunt ameibuka na kutoa kauli kali bila kuuma maneno kwamba, Wema akitangulia kuaga dunia, yeye hatakwenda kumzika kwa maana ya kuuaga mwili wake sanjari na kuomboleza.

KIASA CHA KAULI

Kauli hiyo ya Aunt imekuja siku chache baada ya Wema naye kudaiwa kutoa kauli kama hiyo akisema kwamba, kutokana na urafiki wake na Aunt kufa na kuwa maadui, basi hata akifa, Aunt asiende kumzika.

MSIKIE AUNT ‘LAIVU’

Ijumaa wikienda: Aunt pole kwa kulea mimba! Nina machache sana. Wema amedaiwa kuanika hatima ya ugomvi wenu kwamba, hali ilipofikia hata akifa wewe usiende kumzika. Wewe unasemaje?

Aunt: Kwanza nashangaa taarifa za kwamba nina ugomvi na Wema maana hata hao ndugu zake nimesikia wanaongea mambo kibao.

“Ila mimi sioni kama kuweka picha ya tangazo la shoo ya Zari (Zarinah Hassan) kwenye peji yangu ya Instagram ni kosa. Kwa hiyo kama yeye hataki kuzikwa na mimi, hata mimi nasema sitamzika Wema.

AANZA KUFUNGUKA

”Halafu sidhani kama kuna mtu anaweza kunipangia kitu kwenye peji yangu mwenyewe ambayo nina uamuzi wa kufanya chochote ninachojisikia.

ILIKUWA UTANI, IYOBO ATAJWA

“Mimi sidhani kama hapo kuna ugomvi, maana nilichoandika na kuweka siku hiyo ilikuwa ni utani lakini hata kama yeye na ndugu zake walichukulia ‘siriasi’ basi bado walitakiwa kutambua kuwa, mchumba wangu Iyobo (Moses) ni mfanyakazi halali wa kundi la muziki la Diamond (Nasibu Abdul), hivyo nilikuwa na haki ya kumsapoti kwa asilimia zote maana fedha anazopata kupitia huko ndizo zinazonifanya mimi na familia yangu niishi,” alisema Aunt.

FAMILIA YAWEKA KIKAO

Kufuatia vuguvugu hilo kushika kasi, hivi karibuni familia ya Wema inadaiwa kuweka kikao na kusema kwamba walimuonya ndugu yao huyo siku nyingi kwa kumwambia kuwa, urafiki wake na Aunt ni sawa na ‘spea’ za ki-China kwani waliamini hautadumu kwa sababu ni unafiki tu bora hata alivyokuwa na Kajala Masanja.

Chanzo makini kutoka katika familia ya Wema kimelipenyezea ubuyu Ijumaa Wikienda ambapo kilitiririka:

“Mama Wema kama kawaida yake, alifikia hatua ya kusema kwa sasa hataki tena kumwona mwanaye akirudia urafiki wake na Aunt kwa sababu ni mnafiki.

MAAZIMIO YA KIKAO YAFIKA KWA WEMA

“Maneno hayo ya mama na ndugu wengine, yalifikishwa kwa Wema, akawaelewa na kusema hana haja tena ya kuwa karibu na Aunt hata itokee nini maana hakuna anachomsaidia.”

AUNT TENA, AMWANIKA WEMA SASA

Aunt alipoambiwa kuhusu maazimio ya kikao cha familia ya Wema na jinsi staa huyo alivyoyapokea, alisema:

“Kama familia yake wamefikia hatua ya kuingilia hili, mimi nafikiri sina tatizo maana nina maisha yangu na yeye (Wema) ana maisha yake. Ila tu kama ni ishu ya wazazi, naomba wajue pia mimi sijajizaa wala sijazaliwa na miti, nina ndugu tena wanajitambua kwa kila hali.

“Nikiangalia sababu za ugomvi ni za kibinafsi sana hata hazifai kuingiliwa na mtu, maana haiwezekani kwenye maisha haya eti Wema akinuniana na mtu basi na mimi nimnunie, sijaumbwa hivyo wala sina unafiki huo.

“Kama staili ya maisha ikiwa kila atakayekwazana naye na mimi nimchukie siku wanapoelewana mimi si nitaonekana sifai kote? Wao wafahamu kuwa mimi najitambua wala si wa kuburuzwa hivyo.

“Kama wanasema hawawezi kushiriki lolote kwangu hata mimi sina sababu ya kujipendekeza kwao.

WEMA AZIDI KUCHAMBULIWA

“Hakuna kitu kibaya katika maisha kama kuwa na rafiki ambaye siku zote yeye akikosana na mtu basi na wewe ukosane naye. Mbona mimi maadui zangu yeye ni marafiki zake na wala sijawahi kununa. Iweje sisi tukorofishane na watu yeye aongee nao ila yeye akikorofishana na watu basi hataki kabisa hata kutuona nao?”

WEMA NAYE ATEMA NENO

Baada ya Ijumaa Wikienda kupata fukunyuku hizo lilimsaka Wema kwa maana ya kujiridhisha na kinachodaiwa kusemwa na yeye na familia yake, mambo yalikuwa hivi:

“Yaani hata sitamani kusikia jina la Aunt maana alichokifanya ni bora hata ya Kajala ambaye ishu yake ni ya moja kwa moja. Nashindwa kuliweka wazi sana lakini familia yangu haitaki hata kumsikia kwa jinsi ilivyochukizwa naye.

“Sifikirii kama kuna siku nitakuja kukaa naye tena au kuongea chochote mbele yake maana alichokifanya si cha kunifanyia mimi tuliyeshibana kama mapacha.”

Aunt ‘mama kijacho’ na Wema walikuwa marafiki walioshibana kabla ya kutofautiana baada ya Aunt kutoa sapoti kwa mpenzi wa Diamond, Zari kwenye shoo yake ya Zari All White Party kwa kuposti picha kwenye mtandao iliyoonesha kupigia debe shughuli hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Mlimani City hivi karibuni jambo lililomkera Wema akiamini Aunt ni mnafiki, yuko kwake na kwa mahasimu wake hao.
Chanzo:Global publishers

DIAMOND PLATNUMZ' SUPERHIT SHOW IN LONDON







Yesterday Diamond Platnumz had a successfull music show in London. Here are some photos although they are not clear but we promise to bring to you clear pics when we get them.....


TAZAMA NA KUDOWNLOAD VIDEO MPYA YA "RUBY-Na yule" na VIDEO YA CHEGE-"Mwananyamala" hapa

  Video mpya ya Ruby – Na Yule


Baada ya wimbo wake ‘Na Yule’ kusikika kwenye radio kwa takribani miezi mitatu sasa, mshindi wa Serengeti Super Diva 2014, Ruby ameachia rasmi video ya wimbo huo ambao ni single ya kwanza. Video hiyo imeongozwa na director kutoka Kenya Kevin Bosco Jnr. Itazame hapa. 


Video mpya ya Chege – Mwananyamala


Msanii wa kundi la TMK Wanaume Family, Chege Chigunda a.k.a mtoto wa mama Saidi ametoa video ya wimbo wake mpya uitwao ‘Mwananyamala’. Video hii imefanywa na Adam Juma. Itazame hapa. 

"BATULI AKEMEA TABIA ZA BAADHI YA YA WASANII KUONESHA MATUMBO YAO WAKATI NI WAJAWAZITO"...ASEMA NI USHAMBA ULIYOKITHIRI

 
Batuli Yobnesh Yusuph isn't happy with fellow female celebs who put their baby bump on display on social media. Apparently Globalpublishers had a post on their Instagram account asking whether pregnant women showing off their naked baby bump on social media is fashion or just provincialism(ushamba).

Batuli went to comment by blasting Aunty Ezekiel, Zari and Hamisa Mobeto on the post which had the photos of three celebs. Batuli said it is unacceptable and bad behavior for pregnant women showing off their undressed baby bump. Some fans replied Batuli with negative comments but the actress insisted it is not good and there are good things to praise not those ones. Below is what Batuli said........


Afande Sele: Wabunge Wengi wa Tanzania Wanavuta Mmea



 
Afande Sele kafunguka kupitia ‪#‎YouHeard‬ ya Power Breakfast Clouds Fm na kusema kuwa wabunge wengi wa Tanzania wanamfuata na kumuomba 'Mmea' wakidhania kuwa yeye bado anavuta. "Mimi huwa nawaelekeza kwa washikaji zangu nnaowajua kisha wao wanaenda kuchukua"

Pia amedai kuwa kuna nchi zilizoendelea na zimepitisha matumizi ya 'mmea' na zinaingiza ushuru wa kutosha kupitia mimea hiyo.

WEMA SEPETU AELEZA KWANINI HAMPENDI TENA DIAMOND NA KWANINI ZARI HAMTISHI KWENYE FASHION

 
 


Wema Sepetu hampendi tena Diamond Platnumz na anasema kila anapoukumbua uhusiano wao, anakumbuka mambo mabaya zaidi kuliko mazuri. 


“Hapana simpendi [Diamond], yalishaisha hayo, nilishampendega, niliwahi kumpenda sana, lakini hamna tena, yaani hata sishtuki,” Wema alikiambia kipindi kifupi cha Kabali cha EFM. 


“Nikimkumbuka Diamond most of the things ambavyo ninavikumbuka sio vitu vizuri na ndio maana hata sasa hivi imekuwa hivyo. Vizuri vilikuwepo lakini mtu anaweza akafanya vizuri akaja kufanya kimoja tu kibaya na akaharibu vyote tisa,” aliongeza. 


Katika hatua nyingine Wema alisema Zari the Bosslady hamtishi katika sekta ya fashion. 


“[Zari] hanitishi kwasababu yeye ana taste yake, mimi nina taste yangu, yeye ni Zari mimi ni Wema,” amesema muigizaji huyo. 

“I got my own, I like to play along with anything and she got her own.”

"MWACHENI ALI KIBA AJILIE MAKOMBO" JOKATE NI MAKOMBO TU....DIAMOND



Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amemuita mpenzi wake wa zamani Jokate Mwegelo kuwa ni makombo na kudai kama zilipendwa huyo anatembea na hasimu wake Ali Kiba, hakuna jipya kwani anakula makombo. 



Diamond ametoa kauli hiyo Jumatano iliyopita wakati mwanahabari wetu alipotaka kujua anajisikiaje kuona wapenzi wake wa zamani Jokate na Wema Sepetu ‘Madam’ wanamuunga mkono Ali Kiba. 


Pamoja na kudaiwa kuwa Jokate ana uhusiano wa ‘kimalovee’ na Ali Kiba na mwenyewe kutokubali, ameungana na Wema kuendesha kampeni ya nguvu kwenye mitandao ya kijamii kuhamasisha watu wampigie kura Kiba kwenye Tuzo za Kili 2015 kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kampeni ya kuuangusha ufalme wa Diamond kimuziki. 


Baada ya mwanahabari wetu kuujua ‘mchezo huo’ uliopamba moto kama moto wa kifuu mitandaoni ndipo alipomuuliza Diamond anauzungumziaje ambapo kwanza alikiri kuufahamu na kudai ameudharau maana hauna jipya. 


“Hamna jipya waache waendelee kumpigia kampeni (Kiba) lakini mimi nafanya muziki wangu, mashabiki wanafahamu. Kwa hao watoto wa kike, hakuna kipya kwangu si kimuziki hata maisha yao binafsi. 


“Wema namjua vizuri, Jokate ndiyo usiseme. Mwache huyo Kiba aendelee kula makombo kwa Jokate kama ameamua kipita njia nilizopita si mbaya, inaruhusiwa,” alisema Diamond. 


Jitihada za kumpata Jokate ili aweze kufunguka kuwa anajisikiaje kuitwa makombo na Diamond hazikuzaa matuda kufuatia simu yake kuita bila kupokewa, jitihada zinaendelea.

SHILOLE KIUNO ATOKA AKALI NYINGINE....CHEKI HAPA



Pozi Kali Kutoka kwa Shilole Kiuno Bila Mfupa Akiwa na Shabiki Wake ...

SIWEMA WA NAY WA MITEGO KORTINI




MAJANGA yamezidi kumkuta mzazi mwenzake na Mbongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Siwema Edson ambapo jana alitarajiwa kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza, kujibu shitaka la kujipatia mali kwa njia vitisho.





Mzazi mwenzake na Mbongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Siwema Edson. Siwema anatuhumiwa kujipatia mali kwa kumtishia kigogo mmoja serikalini (jina tunalihifadhi) ambaye inadaiwa alikuwa mchumba wake na baada ya kuachana, mrembo huyo kwa nyakati tofauti akawa anamtishia kuwa ana picha zake za utupu hivyo asipompa fedha ataziweka mitandaoni hivyo kigogo huyo alikuwa akilazimika kumpatia.
Chanzo cha habari hii kimeeleza kwamba, baada ya polisi kujiridhisha na uchunguzi wa madai hayo, waliamua kumpeleka mahakamani ili kujibu shitaka hilo linalomkabili.
“Kesho (jana) wanampandisha mahakamani akajibu shitaka linalomkabili maana polisi tayari wameshamaliza uchunguzi wao hivyo sakata hilo linahamia mahakamani,” kilisema chanzo chetu.
Alipotafutwa Siwema kwa njia ya simu, simu yake iliita bila majibu lakini alipopigiwa msaidizi wake wa dukani aitwaye Zuhura, alisema:
“Dada (Siwema) jana alikuwa polisi hivyo sijajua kama wamempeleka mahakamani au la!”
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi, Charles Mkumbo alikiri kumkamata Siwema kwa kosa la kujipatia mali kwa njia ya vitisho kisha kumuachia kwa dhamana.

BONGO MOVIE: BAADA YA KITAMBO KIREFU WEMA ARUDI MZIGONI AKIWA NA JB



Staa mrembo wa Bongo Movies, Wema Sepetu ameshare nasi kipande kidogo cha video ya kazi mpya inayokwenda kwa jina la Chungu Cha Tatu akiwa na Staa mwenzake, Jacob Stephen 'JB' wakiwa 'lokesheni'.

Kwa muda mrefu sasa Wema Sepetu amekuwa afanyi filamu, Bila shaka mashabiki wake wana hamu kubwa sana ya kumuona tena kwenye filamu.
Source:Udaku Special Blog
Older Posts
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top