
MWENYEKITI
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kata ya Sungaji, Musa
Kombo, amesema, Kata yake haiwataki Wanachama Popo ambao Usiku wanajenga
Mashina ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mchana wanavaa Magwanda
wakijifanya Chadema.
Kombo
alisema, Kama yalivyo maamuzi ya Kamati Kuu ya Chadema, wao pia
wanayatii yaliyoamuliwa na vikao hivyo, kwa hiyo watakuwa wa mwisho kuwa
na Mbereko ya kuwabeba wanachama Popo katika chama chao, ikiwemo Kata
yao.
Kauli
ya Kombo inafuatia kuwepo kwa fununu za Mwanachama, Reuben Sembuche,
aliyekuwa Chadema na kutupa Kadi ya Chama hicho kwa madai ya kukiacha,
lakini hivi karibuni alionekana katika moja ya Mikutano ya Chadema
Wilaya Kata hiyo akihutubu mkotanoni.
Kombo
alisema, “Zipo Taratibu za Chama ambazo mtu akikengeuka kwenye Chama
anapotaka kurejea lazima azifuate ili ajadiliwe na hatimae arejeshwe!
Lakini Kata inashangaa kuona mtu huyo huyo yupo jukwani amerudi
kinyemela na Uongozi wa Kata hauna habar”.
Kombo
aliuasa Uongozi wa Wilaya Mvomero, kuwa Makini sana na Watu ambao kwa
siku za hivi karibuni wamekuwa si watiifu ndani ya Chama, na badala yake
wamekuwa wakitumika vibaya na Upande wa pili ili kukidhoofisha Chadema
kwa Tamaa ya Fedha na Madaraka.
Aidha
Ijumaa Desemba 29, Mwaka huu, Chadema Kata ya Sungaji ilikuwa na Kikao
kujadili na kutathimini Mustakabali wa Mafanikio na Mapungufu ya
Mikutano ya Chama chao iliyofanywa na Wilaya katika Kata ya Sungaji
Vijiji vya Mbogo na Kigugu, ambapo Mapungufu ya ukiukwaji wa Ratiba ya
Mikutano, lilikuwa mojawapo.
Gazeti
hili lilimtafuta Katibu Mwenezi na Kaimu Katibu wa Wilaya, Mohamed
Mrisho, na kumwandikia Ujumbe Mfupi (SMS) kujua iwapo yupo Mwanachama
Popo aliyerejea kinyemela lakini hakutoa ushirikiano, hata hivyo
Mwenyekiti wa Wilaya, Saimanga Kashikashi naye hakujibu Ujumbe Mfupi
alioandikiwa hadi tunakwenda mitamboni.


Post a Comment