SHETANI anazidi kuuatamia ulimwengu! Mama mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Farida mkazi wa Mburahati jijini Dar, amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kudaiwa kumuua mumewe aliyetajwa kwa jina la Amos Joseph kwa kumpiga kwa kukombe kichwani, Ijumaa linaidondosha kama ilivyo.

Amos Joseph enzi za uhai wake.
Akisimulia mbele ya gazeti hili mkasa mzima, mtoa habari hii aliyetajwa kuwa dada wa marehemu anayejulikana kwa jina la Khadija, alisema siku ya tukio kaka yake aliamka asubuhi na kumuaga kuwa anakwenda bondeni kwa mkewe (Farida) kwa kuwa walikuwa nyumba tofauti.
Aliongeza kuwa, muda mfupi baada ya kaka yake kuondoka nyumbani hapo, wifi yake (Farida) alifika nyumbani hapo na kumwambia kuwa kaka yake ameumia sana aende akamuone.
“Muda mfupi, uliingia ujumbe kwenye simu yangu ya mkononi ukisomeka kuwa kaka yangu alikuwa amefariki dunia huku ujumbe huo ukinionya kutolia ili nisimshitue mama,” alisema Khadija.
Marehemu Amoni alizikwa siku chache baada ya kufariki dunia kwenye makaburi ya Mburahati City jijini Dar huku Farida akiwa mikononi mwa polisi kwa upelelezi zaidi.
Post a Comment