Villas-Boas atupiwa virago Tottenham



KOCHA Mkuu wa Tottenham Hotspurs, Andre Villas-Boas, ametimuliwa kazi ikiwa ni siku moja tu baada ya kichapo cha mabao 5-0 kutoka kwa Liverpool.


“Klabu inathibitisha kuwa makubaliano yamefikiwa kuwa Andre Villas-Boas aachishwe kazi,” taarifa ya klabu hiyo ilisema jana Jumatatu mchana.


“Uamuzi huu umechukuliwa kwa faida ya pande zote mbili.”


Tangu juzi Jumapili wadadisi wa masuala ya soka walimtazama Mreno huyo kama ni kocha anayesubiri kufungashiwa virago vyake baada ya kikosi chake kushindwa kutamba kwenye Ligi Kuu England licha ya kutumia pesa nyingi kwenye usajili.


Habari zilisema kwamba Mwenyekiti wa Tottenham, Daniel Levy, ameshamwandaa mrithi wa Villas-Boas na hadi jana Jumatatu mchana alikuwa katika hatua za mwisho za makubaliano na mbadala huyo anayemhitaji.


Tottenham imeshindwa kuonyesha cheche kwenye ligi msimu huu licha ya kufanya usajili mkubwa majira ya kiangazi na kabla ya kuivaa Liverpool ilichapwa mabao 6-0 na Manchester City kwenye Ligi Kuu England wiki tatu zilizopita.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top