Viwango vya ufaulu vinapokinzana na malengo ya elimu, dira ya Taifa





Watanzania tujiulize nchi gani iliwahi kuboresha elimu yake kwa kupunguza viwango vya ufaulu?


Hivi karibuni Serikali ilitoa uamuzi wa aina yake na wa kihistoria kwa kupanga upya viwango vya ufaulu.


Kwa watu wengi tatizo siyo upangaji bali ni madaraja ya ufaulu hayo kupunguzwa alama, hivyo kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye viwango vidogo vya ufaulu barani Afrika na dunia kwa jumla.


Alama hizo zilizotangazwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome zitakuwa kama ifuatavyo: A=75-100, B+=60-74, B=50-59, C=40-49, D=30-39, E=20-29 na F=0-19,


Malengo ya elimu ya Tanzania


Ukweli ni kuwa uamuzi huo unakinzana na malengo ya elimu ya Taifa hili ambayo ni; Mosi, kujenga na kudumisha stadi za kusikiliza, kuzungumza, kusoma, kuandika, kuhesabu, ubunifu na kuwasiliana kwa ufasaha kwa lugha ya Kiswahili na lugha nyingine za kigeni.


Pili, kukuza na kuendeleza mila, desturi na utamaduni wa jamii ya Watanzania. Tatu, kurithisha, kuendeleza na kutumia maarifa, stadi na mielekeo itokanayo na maandishi anuai, sayansi ya jamii, sayansi ya asili, teknolojia na mafunzo ya kazi kuendeleza jamii anamoishi.


Nne, kukuza na kuendeleza moyo wa kujiamini, kudadisi, kutathmini, kufikiri kiyakinifu na kufanya uamuzi wa busara, kuheshimu utu, haki za binadamu na kuchochea utayari wa kufanya kazi kwa bidii kwa maendeleo binafsi na ya Taifa.


Tano, kujenga uwezo na ari ya kujielimisha na utashi wa kuendelea kutafuta maarifa na stadi za kiutendaji. Sita, kujenga na kuendeleza heshima kwa Katiba ya nchi, kuthamini utawala wa sheria na haki za binadamu.


Saba, kujenga uwezo na misingi ya kutambua, kuheshimu na kupenda kufanya kazi kwa bidii na kwa ufanisi. Nane, kukuza ari ya kuyatambua na kuyahifadhi mazingira. Tisa, kujenga na kudumisha misingi ya kuthamini umoja, amani na ushirikiano wa kitaifa na kimataifa.


Kumi, kujenga misingi na ari ya kutambua na kuthamini mchango wa sayansi na teknolojia katika maendeleo ya taifa.


Malengo haya ambayo yako wazi kwenye sera ya elimu, mihtasari ya shule za msingi na sekondari, kwenye mipango mikubwa ya kitaifa kama MKUKUTA, MMEM, MMES, yametupwa kapuni. Sasa utashi wa watu na ghiliba za kisiasa ndizo zinazoamua hatma ya nchi yetu.CHANZO MWANANCH

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top