Kikwete afunga mjadala wa gesi



Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Sheikh Ahmed Jongo alipowasili kufungua kongamano la viongozi wa dini lililokuwa likijadili ‘Rasilimali za Gesi, Mafuta na Madini kwa Amani na Maendeleo ya Watanzania’ jijini Dar es Salaam jana. Picha na Venance Nestory

Dar es Salaam: Rais Jakaya Kikwete amefunga mjadala wa wafanyabiashara wazawa wanaotaka kupewa kipaumbele katika uwekezaji wa sekta ya gesi akisema Shirika la Maendeleo la Petroli(TPDC) linajitosheleza kuwasaidia Watanzania wanufaike na rasilimali hiyo.


Katika kipindi cha miaka miwili, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ameshikilia kuwa hakuna Watanzania wenye uwezo wa utafutaji, uchimbaji na uzalishaji, jambo ambalo linapingwa vikali na wafanyabiashara wazawa.


Akizungumza jana wakati wa Kongamano la Viongozi wa Dini kuhusu rasilimali ya gesi, mafuta na madini kwa ajili ya amani na maendeleo ya taifa, Rais Jakaya Kikwete alisema hakuna kampuni nchini yenye dhamana ya kupata mikopo kwa ajili ya kuwekeza katika sekta hiyo.


“Kampuni za kigeni zenye mitaji mikubwa zinafanikiwa kupata mikopo kwa kuwa zina dhamana inayowasaidia kupata mikopo kwenye mabenki,” alisema.


Hata hivyo, Rais Kikwete alisema kama kuna kampuni za Watanzania zinatakiwa kushirikiana na wawekezaji watapaswa kufuata taratibu zilizowekwa.


Rais Kikwete alisema uwekezaji kwenye sekta ya mafuta ni kama mchezo wa kamari kwani mtu anaweza kuwekeza fedha nyingi katika utafutaji wa gesi na asipate kitu.


“Ni kampuni gani Tanzania ambayo itakuwa tayari kucheza kamari?” alihoji Rais Kikwete.


Alisema ndio maana Serikali imeona ni vizuri iandae mpango wa kuiwezesha TPDC kuingia kwenye shughuli za gesi badala ya kuwa kutoa leseni tu.


“Tunataka siku moja TPDC iwe na uwezo wa kuwauzia hisa Watanzania iwe kama kampuni kubwa za Statoil(Norway) na Petro Plus(Brazil) zinazoendeshwa na Serikali zao,” alisema.


Rais Kikwete alisema baada ya kuliwezesha shirika hilo, Watanzania watanufaika kwa kiwango kikubwa tofauti na kutoa kipaumbele kwa kampuni binafsi za Watanzania.


Washiriki watoa maoni tofauti


Mwakilishi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Dk Charles Kitima alipinga kongamano hilo kufanyika sasa kwani alieleza lilipaswa kufanyika miaka mitano iliyopita na sio sasa wakati ambapo shughuli za uchimbaji wa gesi zinakaribia kuanza.
 
Chanzohttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Kikwete-afunga-mjadala-wa-gesi/-/1597296/2155440/-/quu865z/-/index.html

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top