HATI YA MUUNGANO YALETA UTATA BUNGE LAKATIBA: soma kwa habari kamil





click hapa kungalia video
video

Dodoma. Majadiliano makali yameibuka katika Bunge Maalum la Katiba, huku wajumbe wakilumbana kuhusu marekebisho ya kanuni ili kuwezesha nyaraka mbalimbali, ikiwemo ‘Hati ya Muungano’, kupatikana kwa urahisi.


Hoja hiyo iliibuliwa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema), aliyeshauri kanuni ya 4 ya kuliendesha Bunge hilo Maalum irekebishwe ili kuwawezesha wajumbe kupata nyaraka au taarifa yeyote wanayoihitaji katika kutekeleza kazi iliyowaleta Dodoma kwa ufanisi.


Kauli hiyo ilipingwa vikali na Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole-Sandeka (CCM) aliyetahadharisha kuwa hizo zisije zikawa njama za kulazimisha “Hati Ya Muungano” ianikwe hadharani. Akijibu hoja hizo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Othman Masoud, ameliambia baraza la Katiba kuwa Hati ya Muungano ipo katika sheria hivyo wajumbe wanaweza kuipata kwa uhuru kabisa kwani ni sehemu ya nyaraka za umma

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top