Dodoma. Ni vigumu kueleza matukio yote yaliyotawala kauli na hisia za wengi kwa wiki nzima mjini Dodoma bila kuangalia michango ya baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba.
Michango hiyo ya mawazo katika mjadala kuhusu rasimu ya kanuni zinazopaswa kuongoza kikao kwa siku 70 za kikao hicho, baadhi yake zilikuwa kali.
Zifuatazo ni baadhi ya kauli hizo:
Mchungaji Christopher Mtikila
Mtikila, ambaye ni mwenyekiti wa Democratic Party (DP), alitumia dakika tano kutoa somo kwa wajumbe wa Bunge hilo kuhusu umuhimu wa kupiga kura ya siri badala ya ile ya wazi.
Anasema haki ya kupiga kura kwa siri haitofautiani na haki ya mtu kuwa na miguu miwili na kwamba itashangaza akitokea mtawala akaamuru kila mtu awe na mguu mmoja, halafu watu wakakaa kujadili.
“Wote tutaonekana tuna matatizo ya akili,” alisema Mch. Mtikila.
Alisema Bunge Maalumu la Katiba litaingia katika hatia na aibu kwa kujadili mambo ya msingi ya kidemokrasia ambayo pia yameainishwa katika katiba ya sasa, likiwamo suala hilo la kura ya siri.
“Mwenyekiti (akimlenga Pandu Ameir Kificho) tumekuchagua kwa kura ya siri siyo kwamba tulikuwa wajinga kuliko wenzetu, hapana! Ni ‘democratic civility’ (ustaarabu wa kidemokrasia),” alisema.
“Ni aibu waheshimiwa na hii nasema si jambo la mjadala kuna vitu vya kujadili, lakini si haki ya kupiga kura kwa siri. Hii ni haki ya msingi ya kidemokrasia,” alisema.
Esther Bulaya (Viti Maalumu-CCM)
Bulaya, tofuti na wajumbe wenzake wengi kutoka chama tawala (CCM), alionekana kutoa mchango uliogusa hisia za wengi hasa pale alipoeleza bayana kuwa hayuko tayari kuona ukandamizaji unafanyika kumlazimisha apige kura ya wazi.click hapa kuendelea


Post a Comment