Matukio ya jana usiku katika office za CCM: Mkutano Mkuu CCM waahirishwa hadi saa 4 asubuhi




12:43: Baada ya upigaji kura kwa wagombea wote watatu ili kumpata mmoja, Rais Jakaya Kikwete ameahirisha Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa hadi saa nne asubuhi.


12:11 Mgombea wa mwisho wa CCM Dk John Pombe Magufuli amemaliza kujinadi mbele ya Mkutano mkuu wa CCM.


amesisitiza kuwa atakwenda kuilinda na kuisimamia ilani ya Chama cha Mapinduzi.


Amesema ataulinda Muungano na kuhakikisha kuwa anakisaidia Chama Cha Mapinduzi kupata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba


12:01 Mgombea Dk Asha-Rose Migiro amemaliza kujinadi kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM akieleza hisia zake na nia yake thabiti ya kutaka kuliongoza taifa la Tanzania


Amesema atahakikisha anaulinda umoja wa kitaifa, kuulinda Muungano, Kuyalinda kipekee Mapinduzi ya Zanzibar, kupata Katiba Imara, pamoja na kusimamia yale yote yaliyomo kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi.


11:51 Mgombea wa kwanza wa nafasi ya urais Balozi Amina Salum Ali ameanza kujinadi mbele ya wajumbe wa Mkutano mkuu wa CCM.


Amezungumzia suala la kulinda Muungano, kutekeleza yale mazuri na kuyatafutia ufumbuzi yale yote yaliyoachwa na Rais Kikwete. pia kusimamia majukumu ya chama imara kitakachokuwa na viongozi bora wanaosimamia maadili Serikalini.


Hakuulizwa swali lolote


11:37: Rais Jakaya Kikwete amemaliza kuzungumza na wajumbe wa mkutano mkuu mjini Dodoma akimfagilia Katibu Mkuu wa chama hicho Abdulrahman Kinana kwa madai kuwa amekifikisha chama katika eneo salama.


10: 59 Rais Jakaya Kikwete na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, anaanza kuzungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho


10:56 Mkutano Mkuu wa CCM umeanza mjini Dodoma na Muda huu Katibu Mkuu wa chama HichoAbdulrahman Kinana anazungumza. Pamoja na mambo mengine Anaeleza jinsi walivyoweza kufanya ziara katika mikoa yote nchi.read more,,,,,,,,,,,

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top