Magufuli kutumbua majipu ya kina Museveni, Kagame EAC

magufuli

MWENYEKITI wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Rais Dk. John Magufuli, amehamishia kampeni yake ya kubana matumizi na kutumbua majipu kwa watendaji wa sekretarieti ya jumuiya hiyo watakaokiuka maadili ya kazi.
Amesema ikiwa kuna jambo litatokea kwa mtendaji yeyote, ataitisha kikao cha wakuu wa nchi za jumuiya hiyo na kuwaeleza suala hilo na ikiwezekana watendaji hao watatumbuliwa katika nchi zao.
Msimamo huo aliutoa jijini Arusha jana wakati mkutano wa 17 wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, uliofanyika Hoteli ya Ngurudoto, ambako aliongezewa muda wa mwaka mmoja wa kuongoza jumuiya hiyo,baada ya wakuu wa nchi hizo kuridhia kwa kauli moja.
Kauli hiyo aliitoa mbele ya marais wa nchi wanachama wa jumuiy hiyo, Rais Yoweri Museveni (Uganda), Paul Kagame (Rwanda), Uhuru Kenyatta (Kenya), Makamu wa Pili wa Rais wa Burundi, Joseph Butole na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.
Aliwataka watendaji wa sekretarieti kuhakikisha wanabana matumizi katika utendaji kazi wao wa kila siku.
“Nitahakikisha ninawafuatilia kwelikweli na endapo atabainika mtendaji wa sekretarieti anayekwenda kinyume na maadili, nitatoa taarifa kwa mkuu wake wa nchi ili atumbuliwe jipu.read more

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top