Wajumbe Kamati Kuu CHADEMA wamuonya Zitto.



Baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu CHADEMA wamemuonya aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe kwa ukiukwaji wa waziwazi wa taratibu za chama hicho.
Wakizungumza kwa nyakati Tofauti wajumbe hao wameshangazwa na kitendo cha Zitto Kabwe kujiandalia ziara zenye mwelekeo hasi kwa chama hicho.
Ikumbukwe kwamba Zitto amefukuzwa nafasi zote za Uongozi ndani ya Chadema na yeye ni mbunge tu wa Kigoma Kaskazini huku akisubiri huruma ya Kamati Kuu kuhusu uanachama wake.
Kilichoshangaza zaidi ni kitendo cha Zitto Kabwe kufanya ziara Jimbo la Kasulu bila kutaarifu Chama huku mashabiki wake wakiutumia mkutano huo kukashifu chama na viongozi wake.
Kitendo kinachofanyika hakikubaliki na ni ukiukwaji mkubwa wa Kanuni na taratibu za chama.
Katika hali ya kuonyesha kinachofanywa ni mkakati wa kuangamiza Chadema Gazeti la Jamboleo Toleo la Jumapili linalomilikiwa na Kada wa CCM katika habari kuu limeandika "Zitto aimaliza CHADEMA" likiripoti yanayotokea Kigoma.

1 comments:

kwa hakika kitendo cha kufanya ziara mikoani ni cha kipuuzi na viongozi wa chadema wanapaswa kuyaspopisha haraka hadi yapate kibali cha chama. akitaka kufanya hivyo aombe kibali au ajiondoe chadema ili atumie muda huo akiwa nje ya chadema. kwa kuwa ni mwanachama wa chadema athibitiwe au atimuliwe maana anagharimiwa na ccm na vyama pinzani vya chadema. please be very string top leaders

Reply

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top