KATIBU Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amegoma kutambua uteuzi aliofanya Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu wa Mkurugenzi wa Wanyamapori, Paul Sarakikya kwa kumwondoa, Profesa Alexander Songorwa.
Nyalandu alitangaza uteuzi wake huo Jumatatu wiki hii, akisema ni uamuzi unaotekeleza matakwa ya Ripoti ya Kamati ya Bunge, kuhusu matokeo ya Operesheni Tokomeza.
Mbali na Sarakikya, aliwateua Dk. Charles Mulokozi kuchukua nafasi ya Mkurugenzi Msaidizi wa Matumizi Endelevu ya Wanyamapori na Julius Kibebe kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Uzuiaji-Ujangili.
Kwa mujibu taarifa za uhakika kutoka vyanzo vyetu vya habari, Nyalandu alifanya uteuzi wake huo bila kumshirikisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Maimuma Tarishi, ambaye alikuwa safarini mkoani Ruvuma na ambaye kwa kuzingatia taratibu za utumishi serikalini ndiye mhusika chini ya usimamizi wa Katibu Mkuu Kiongozi.
Taarifa za uhakika zilizopatikana muda mfupi kabla ya kwenda mitamboni, zilieleza kwamba Balozi Sefue alifanya mawasiliano na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Selestine Gesimba, kuuliza kilichotokea, naye akamjibu hakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu suala hilo.
Ni kutokana na hali hiyo, maelekezo yalitolewa kwamba, Profesa Songorwa na Jafari Kidegheso waandike barua za likizo na kukaimisha majukumu yao kwa watendaji wa ngazi za chini, ambao ni utaratibu wa kawaida kwa watu wa juu wanapokwenda likizo kukaimisha majukumu yao kwa watendaji wa chini yao.
“Hili suala limekataliwa na Katibu Mkuu Kiongozi, amepiga simu hapa akamuuliza Naibu Katibu Mkuu imekuwaje naye akamjibu hajui. Katibu Mkuu ameelekeza wahusika waandike barua za kwenda likizo na kukaimisha watendaji wa chini na hatambui mabadiliko yaliyofanywa na Waziri ambaye kimsingi hana mamlaka hayo,” kilieleza chanzo chetu cha habari.
Katika hatua nyingine, Raia Mwema limeelezwa kwamba hata Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Maimuna Tarishi alishitushwa na alichokifanya Nyalandu bila kumshirikisha.
Hii si mara ya kwanza kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kukumbwa na mkasa wa aina hiyo. Mwaka 2007, aliyekuwa waziri, Anthony Diallo alimwondoa madarakani aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Emmanuel Severe, ambaye yeye tofauti na akina Songorwa, alikuwa akituhumiwa kuhusika katika mtandao wa ufisadi uliokuwa ukihusisha uwindaji wanyama na vitalu vya uwindaji.
Katika hatua yake hiyo, Diallo alikumbana na upinzani mkali kutoka kwa Severe ambaye alimwambia Diallo kwamba hakuwa na mamlaka ya kumwondoa kazini.
Severe alikuwa na ujasiri kiasi cha kutamka hadharani kwamba Diallo ataondoka kwanza yeye wizarani hapo kabla yake. Kutokana na mvutano huo, aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo alifuta uamuzi huo wa Diallo kwa maelezo kwamba si mamlaka yake.
Severe aliendelea kubaki wizarani kwa muda mfupi kabla ya Rais Jakaya Kikwete kuidhinisha kuondoka kwake na kumhamishia Chuo cha Utalii Mweka, mkoani Kilimanjaro. Diallo naye hakukaa sana wizrani hapo More...........


Post a Comment